MALKIA WA USHUHUDA DR TUMAIN MSOWOYA AWAGUSA WENGI
Mariam kilyenyi amtaja Dr Tumaini msowoya kama Malkia wa ushuhuda Tanzania asema nyimbo zake na harakati zake Dr Tumaini zimejaaa ushuhuda mwingi ambao umegusa watanzania wengi
Pichani akionekana MWIMBAJI MARIAM KILYENYI akiwa na DR TUMAIN MSOWOYA katika hafla fupi ya kuwania tuzo.
Kwa ufupi: MWIMBAJI MARIAM KILYINYI ni MWIMBAJI anaye sifika kwa. Jina la MAMA WA UPENDO
Kutokana na kawaidayake ya kuwapenda na kuwapa ushilikiano Mkubwa waimbaji wenzake na sasa MWIMBAJI huyu anakaribia kuzindua album yake Mpya tarehe 02/mwezi 12 /mwahahuu 2018 dani ya kanisa la KKKT SINZA jiji la dar es salama na inataraji kuwa siku kubwa na ya kipekee kutokana na upendo wake kwa waimbaji wenzake
watu mashuhuri kutoka nje na ndani ya nchi wameendelee kudhibitisha kuwepo sikuhiyo ikiwemo UTUKUFU LABEL kutoka nchini ZAMBIA ambapo ndani yake kuna waimbaji kutoka KENYA, NIGERIA, na AFRICA YA KUSINI
Karibuni Sana Na asante kwa kuungana nasi karibu ujifunze neno la Mungu popote ulipo pia waweza kuwasiliana nasi kupitia +255622510770 Call 0628080839 WhatsApp 0744318744 Email address godfreymgaya20@gmail.com
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo NENO LA LEO. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 24 Oktoba 2018
FAIDA KUMI NA MBILI ZA MAOMBI
MOJA: Maombi yanaimarisha uhusiano wa mtu na Mungu; Maombi ni mawasiliano baina ya mwanadamu na Mungu au ni njia ambayo tunaweza kuwasiliana na Mungu. Naamini unafahamu kuwa mawasiliano yanaongeza uhusiano wa mtu na mtu, hata wewe ni shahidi katika hili unaweza ukawa na ndugu wengi sana au marafiki wengi sana lakini yule ambaye anawasiliana na wewe mara kwa mara huyo ndiye anayeukuza ukaribu baina yenu kuliko wengine.
Ukweli wa mambo ni kwamba uhusiano wa mtu na mtu unaanzishwa kwa mawasiliano na vile vile unaweza ukapungua au hata ukafa kabisa kwa kukosa mawasiliano ya mara kwa mara. Mawasiliano ndio yanayofanya mahusiano yawe hai na yenye afya na ndio yanayowafanya watu wengi kuwa karibu. Tunapokuwa tunaomba mara kwa mara uhusiano wetu na Mungu unakuwa kwa kasi sana kuzidi yule asiyeomba, au yule anayeomba mara moja moja au yule anayeomba kwa viwango vya juu zaidi. Na kama tujuavyo, kadiri uhusiano wa mtu na mtu unavyokuwa na kuongekezeka ndivyo wanavyoweza kushirikishana mambo mengi zaidi.
MBILI; Maombi yanaweza kubadili maamuzi ya Mungu aliyoyapanga kwa taifa au kwa mtu ili afanye sawa sawa na vile wewe unataka lakini sawa sawa na kusudi lake; “Siku hizo Hezekia akaugua, akawa katika hatari ya kufa. Isaya, nabii, mwana wa Amozi, akamjia akamwambia, Bwana asema hivi, Tengeza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona. Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana akasema, Nakusihi, Bwana, ukumbuke sasa, jinsi nilivyokwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana. Ikawa, kabla Isaya hajatoka katika mji wa kati, neno la Bwana likamjia, kusema, Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, Bwana, Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama, nitakuponya; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa Bwana.” (2 FAL. 20:1-5). Hezekia alijua aljua na aliamini kuwa maombi yanaweza kubadili maamuzi ya Mungu la sivyo asingeomba. Soma pia Yona 3:1-10.
Kama maombi yanaweza kumshawishi Mungu kubadilisha maamuzi basi maombi yanaweza kutumika kubadilisha maamuzi ya mtu, ipo mifano mingi ya kibiblia inayoelezea juu ya maamuzi ya wanadamu yaliyobadilishwa baada ya maombi, hapo juu nimezungumzia tu mifano ya maombi yaliyobadilisha maamuzi ya Mungu. Maombi yanaweza kugeuza maamuzi ya yule bosi wako pale kazini, maombi yanaweza yakabadili maamuzi ya watawala. Maombi yanaweza kubadili matamko na laana za ukoo, inawezekana familia inapitia kwenye vifungo vya umaskini mkubwa pamoja na kufanya kazi kwa juhudi, roho za magonjwa, vifungo vya kutokuoa au kutokuolewa, kwa njia ya maombi mwamini anaweza kubadili laana zote na kuwa Baraka.
TATU: Maombi yanatupa nguvu ya kutoingia majaribuni ; Yesu aliwawaambia wanafunzi wake maneno haya kwa uzito sana baada ya kuona wanafunzi hawana maisha ya maombi! Walikuwa wanafikiri jukumu la kuomba ni la Yesu tu! Kama sisi tunavyofikiri sasa, kwamba jukumu la kuomba ni la watu fulani tu, na si la kwetu.
Kila mahali ambapo Yesu alikuwa anaomba wanafunzi wake ambao leo tunawatambua kama mitume! Walikuwa hawana maisha ya maombi. Angalia hapa Luka 9:28-32, “Baada ya maneno hayo yapata saa nane, akawatwaa Petro na Yohana na Yakobo, akapanda mlimani ili kuomba (Hilo ndio lilikuwa lengo lakini angalia matokeo yake).Ikawa katika kusali kwake sura ya uso wake ikageuka…” (Hapa Yesu anaomba peke yake wale aliopanda nao walishamwacha walikuwa na usingizi). Petro na wale waliokuwa pamoja naye walikuwa wamelemewa na usingizi: lakini walipokwisha amka…”
Inaonyesha wazi walikuwa wamelala wakati Yesu anaomba! Walikuwa wanaona shida kuomba kama sisi tunavyoona shida! Lakini tatizo lilikuwa linajirudia tena na tena kwa wanafunzi mpaka ikabidi Yesu awaambie madhara ya kutokuwa na maisha ya maombi! Hapa lilikuwa tukio jingine sio lile la mlimani! Mathayo 26:40-41, “Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, je! Hamkuweza kukesha nami hata saa moja? Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni.
NNE; Maombi yanaondoa vikwazo au vipingamizi vyote: “Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.” (Marko 11:23-24).
TANO; Maombi hugeuza mioyo na tabia ya watu wengine; “Ndipo mfalme akaniambia, Una haja gani unayotaka kuniomba? Basi nikamwomba Mungu wa mbinguni. Nikamwambia mfalme, Mfalme akiona vema, na ikiwa mimi, mtumishi wako, nimepata kibali machoni pako, tafadhali unipeleke mpaka Yuda, niuendee mji wa makaburi ya baba zangu, nipate kuujenga. Mfalme akaniuliza, (malkia naye ameketi karibu naye), Safari yako itakuwa ya siku ngapi? Nawe utarudi lini? Hivyo mfalme akaona vema kunipeleka; nami nikampa muda. Tena nikamwambia mfalme, Mfalme akiona vema, na nipewe nyaraka kwa maliwali walio ng'ambo ya Mto, ili waniache kupita mpaka nifike Yuda; nipewe na waraka kwa Asafu, mwenye kuutunza mwitu wa mfalme, ili anipe miti ya kufanyizia boriti kwa malango ya ngome ya nyumba, na kwa ukuta wa mji; na kwa nyumba ile nitakayoingia mimi. Naye mfalme akanipa, kama mkono mwema wa Mungu wangu ulivyokuwa juu yangu.” (Nehemia 2:4-8).
SITA; Maombi ni njia ya uponyaji wa kimwili na kiroho; “Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana. Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa.” (Yakobo 5:14-15).
SABA; Maombi huleta msukumo wa kiroho na kumtia mtu nguvu wakati mtu fulani anapokabiliwa na hali ya kushindwa: “Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni; mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu; mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha; (Wakolosai 1:9-11).
NANE; Maombi hufungua milango ya nguvu za Mungu zisizo za kawaida katika maisha yetu: Maombi yanaachilia mwaliko kwa Mungu wetu kutenda kazi katika ulimwengu wetu. Kwa ujumla, maombi ni njia ya kuita nguvu ya Kimungu ili ikatende kazi katika eneo kusudiwa. “Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa.”(MDO 16:25-26)
TISA; Maombi ni njia Mungu aliyoichagua kuzuia nguvu na utendaji kazi wa shetani duniani; “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho… kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote (EFES. 6:12, 18)
KUMI; Kwa njia ya maombi unaweza kuwa mahali kiroho ambapo huwezi kuwa kimwili: Kwa njia ya Maombi unaweza ukasafiri mapaka mkoa mwingine na ukaenda kufanya shughuli za kihuduma huko.
KUMI NA MOJA; Maombi yanakuwezesha kushiriki maamuzi mbali mbali pamoja na Mungu kwenye ulimwengu wa roho: Lakini ndugu yangu nikuambie ukweli maombi ni njia nzuri sana ambayo unashiriki moja kwa moja maamuzi ya mambo mengi katika jamii unayoishi. Inawezekana ni katika familia, au kanisani, au kama ni mtaani kwako, kama ni katika nchi yako na kadhalika. Mungu ametuweka kama mawakili katika maeneo yetu tulipo. Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya; wala msimwache akae kimya, mpaka atakapoufanya imara Yerusalemu, na kuufanya kuwa sifa duniani.”(ISA. 62:6-7)
WARUMI 8:28, " Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. "
KUMI NA MBILI; Kwa maombi yako ingia katika ulimwengu wa roho ili ubadili hali ya ulimwengu wa kimwili: Ulimwengu wa roho ndio mkuu zaidi kuliko ulimwengu wa mwili. Ulimwengu wa roho ndio unautawala ulimwengu wa mwili. Dunia na vyote vyenye kuonekana vimetokea kutokana na ulimwengu ule usioonekana. kila jambo linalotekea katika ulimwengu wa mwili limeanzia katika ulimwengu wa roho. Kufaulu na kushindwa kwetu kote, kabla ya kudhihirika katika ulimwengu wa mwili, kuna kuwa kumepangwa na kutekelezwa katika ulimwengu wa roho. Biblia inasema; “mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo” (3 YOH. 1:2). Hii inamaanisha kwamba mafanikio yetu ya kweli kimwili yanategemea mafanikio yetu ya kiroho. Ni katika ulimwengu wa roho ndiko tunakosimama au kuanguka, tunakoshinda au kushindwa. Adui akitaka kukudhibiti, anamdhibiti roho yako, ukishindwa kufanikiwa rohoni, huwezi kufanikiwa mwilini.

Alhamisi, 13 Septemba 2018
💐🌺🏒🌾🌴🌴KESHA LA ASUBUHI LEO SEPTEMBER 14/2018🌻🌻🌷⛅🌴ISAYA🌾🌾

Naye akaniambia, Enenda, ukawaambie watu hawa, Fulizeni kusikia, lakini msifahamu; fulizeni kutazama, lakini msione. Uunoneshe moyo wa watu hawa, ukayatie uzito masikio yao, ukayafumbe macho yao; wasije wakaona kwa macho yao, na kusikia kwa masikio yao, na kufahamu kwa mioyo yao, na kurejea na kuponywa. Isaya 6:9, 10.
K
azi ya Nabii huyu ilikuwa dhahiri; alipaswa kuinua sauti yake dhidi ya maovu yaliyoenea. Lakini aliogopa kutekeleza kazi hii pasipo kupewa uhakikisho wa tumaini. “Ee Bwana, hata lini?” (Isaya 6:11) aliuliza. Je asiwepo ye yote miongoni mwa wateule wako atakayeelewa, na kutubu, apate kuponywa?
Mzigo wa roho yake kwa niaba ya Yuda wanaopotoka haukubebwa bure. Utume wake usingelikosa kabisa matunda. Lakini bado maovu ambayo yalikuwa yakiongezeka kwa vizazi vingi yasingeondolewa katika siku zake. Katika maisha yake yote anapaswa kuwa mwalimu jasiri, mwenye uvumilivu-nabii wa matumaini pia wa hukumu. Kusudi la Mungu litakapotimilizwa hatimaye, matunda kamili ya juhudi zake, na ya kazi za wajumbe waaminifu wote wa Mungu, yataonekana. Masalia yataokolewa. Ili kwamba hili lipate kutokea, ujumbe wa onyo na kusihi ulipaswa kutolewa kwa waasi, Bwana alitamka, “Hata miji itakapokuwa ukiwa, haina wenyeji, na nyumba zitakapokuwa hazina watu, na nchi hii itakapokuwa ganjo kabisa; hata Bwana atakapowahamisha watu waende mbali sana, na mahame yatakapokuwa mengi ndani ya nchi” (aya 11, 12).
Hukumu nzito zilikuwa ziwaangukie wasiotubu hawa-vita, uhamisho, ukandamizaji, kupoteza mamlaka na heshima miongoni mwa mataifa-haya yote yalikuwa yaje ili kwamba wale ambao wangetambua ndani yake mkono wa Mungu waliyemkosea wapate kuongozwa kutubu. Makabila kumi ya kaskazini yalikaribia kutawanywa miongoni mwa mataifa, na miji yao kuachwa ukiwa; hata Yerusalemu hatimaye ilikuwa ianguke, na Yuda ilikuwa ichukuliwe mateka kwenda nje; hata hivyo bado Nchi ya Ahadi haikupaswa kubaki ikiwa imetupwa milele. -Review and Herald, March 11, 1915. 🌿🌿🍀BARIKIWENI

Jumanne, 4 Septemba 2018
TEMBEA KATIKA IMANI ILI USHINDE YOTE
Biblia katika kitabu cha Mathayo 17:18 inasema‘ ..Ni kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana amini nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. Hii ni habari ya yule kijana aliyekuwa na pepo bubu na kiziwi, mzazi wake akamleta kwa wanafunzi wa Yesu wamwombee. Biblia inatueleza kwamba wanafunzi walijaribu kumtoa yule pepo wasiweze, wakati huo Yesu alikuwa amepanda Mlimani kwenda kuomba. Yesu aliporudi alielezwa kilichotokea, akawakemea wanafunzi wake na kisha akamuombea yule kijana akapona. Baadaye wanafunzi wa Yesu wakamuuliza, kwa nini sisi hatukuweza kumtoa yule pepo. Ndipo Yesu akawajibu akasema ‘Ni kwa sababu ya upungufu wa imani yenu… Neno upungufu lina ya isiyo – tosheleza, yaani imani yao ilikuwa ina upungufu na kwa hiyo wasingeweza kumtoa yule pepo. Jambo ninalotaka tuliangalie ni kwamba kwa kuwa tatizo lilikuwa ni upungufu wa imani yao, ina maana walitakiwa kuongeza imani yao wakati wanaendelea kukemea. Sasa swali muhimu ni je wangeongezaje imani yao wakati wako kwenye jaribu/vitani?. Naam licha ya swali hili kuna maswali mengine ambayo ni muhimu kuyatafakari ili tuweze kuwa na ufahamu mzuri wa imani. Je upungufu huu wa imani kwa wanafunzi walikuwa nao kabla hawajaanza kukemea yule pepo au ulikuja wakati wanaendelea kuomba. Naam Yesu anatuonyesha kwamba kosa la hawa wandugu wenzetu lilikuwa upungufu wa imani yao? Ni kwa namna gani walikuwa na upungufu wa imani? Biblia katika Waebrania 11:1 inaeleza kwamba ‘imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyoonekana’ . Kwa hiyo endapo Yesu alisema ni kwa sababu ya upungufu wa imani yao ina maana ndani yao walipungukiwa uhakika wa kile walichokitarajia, ambacho ni kufunguliwa/kuponywa kwa kijana mwenye pepo. Naam upungufu wao wa imani ulitokana na mashaka juu ya uhakika wa yule kijana kufunguliwa. Nini kilipelekea wao kuingiza hofu/mashaka? Kukosekana kwa dalili za kijana kufunguliwa – Ni imani yangu kwamba wanafunzi walipoanza kukemea walikuwa na uhakika kwamba Yule kijana atafunguliwa. Naam kadri walivyoendelea kuomba na kuona kwamba hakuna mabadiliko ya aina yoyote kwa mgonjwa yule ndipo hofu/mashaka yakawaingia mioyoni mwao. Maneno ya kusikia – Ikumbukwe kwamba chanzo cha imani yoyote ni kusikia (Warumi 10:17)? Kumbuka wakati wanendelea kuomba kulikuwa kuna kundi kubwa la watu ambao walikuwa wanamsubiri Yesu pamoja nao. Hivyo huenda wakati wanafunzi wanaaendelea kuomba walisikia watu wakisema, wanafunzi wa Yohana wenyewe walishindwa kumuombea, wao wataweza, wamejaribu watumishi wa kila aina wameshindwa, huyu hawezekani anasubiri kifo, naam haya yote yakapunguza uhakika ndani yao kwamba kwa jina la Yesu yule kijana anaweza kupona. Maneno yao wenyewe – Biblia haituelezi namna/approach waliyoitumia kuomba/kukemea. Huenda walianza kuomba mmoja mmoja/ au waliomba wachache na mwishowe ndipo wakaomba kama kundi. Kwenye kundi lolote kuna mengi, huenda walipokemea kwa muda kadhaa na bila kijana kuonyesha dalili za kupona baadhi ya wanafunzi wakaingiwa na hofu na wakawaambukiza na wengine na hivyo kushindwa kumtoa pepo. Hebu jaribu kufikiri mtu kama Yuda Iskariote alikuwa anafanya nini wakati wenzake wanakemea? Nini cha kufanya? Hofu/mashaka ni silaha kubwa sana ambayo Shetani huitumia kuwafanya watu washindwe kupata majibu ya maombi/miujiza yao kutoka kwa Mungu. Shetani anafahamu kwamba imeandikwa ‘Mwenye haki wangu ataishi kwa imani, naye akisstasita roho yangu haina furaha naye’ (Wabrania 10:38). Hivyo ili kuharibu/kuondoa imani ya mtu kwa Mungu, silaha anayotumia ni kuingiza mashaka moyoni mwake dhidi ya ahadi za Mungu/neno la Mungu kwenye maisha yake. Yesu aliwaambia hivi wanafunzi wake ‘… amini nawaambia yeyote atakayeuambia mlima huu ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake’ (Marko 11:22). Mpenzi msomaji kamwe usimruhusu Shetani kwa kutumia silaha hii ya mashaka azuie baraka zako na wale wanaokuhusu maishani mwako. Haijalishi jaribu limesimama mbele yako kwa kiwango gani usiondoe imani yako juu ya kile ambacho Yesu amekisema kwenye neno lake juu yako. Naam Mungu wetu si mtu hata aseme uongo, ahadi zake ni amina na kweli. Naam katikati ya jaribu/changamoto wewe ongeza imani yako kwa kupambana na roho ya mashaka/hofu, naam tumia Biblia ili ikuongoze kukupa mistari ambayo itakuongezea uhakika wa kufanikiwa katika lile ulifanyalo. Zaidi kuwa makini na maneno ya kusikia kwa habari ya imani yako. Wanafunzi wa Yesu walipaswa kutokujali maneno ya kusikia kutoka kwa watu, au kwa wenzao walioingia mashaka, naam walipswa kudumu kuamini kwamba kijana atapona naam ingekuwa hivyo. Je si unakumbuka habari za Petro alivyoambiwa na Yesu atembee juu ya maji. Awali alianza vema na akatembea hatua kadhaa juu ya maji. Biblia inasema dhoruba ilipompiga akaona shaka na kuanza kuzama. Kwa nini alizama? si kwa sababu Yesu hakuwepo, bali ni kwa sababu aliona shaka. Naam kitu kilichopungua kwenye imani ya wanafunzi, ni uhakika kwamba yule kijana atapona. Na kilichopelekea upungufu wao wa imani, si kutokumwamini/kumjua Yesu, bali ni kuruhusu hofu ichukue nafasi ya imani/uhakika waliokuwa nao kwamba yule mgonjwa atapona. Naam kwa mara nyingine tena ‘usirihusu hofu iharibu muujiza/future yako’ . Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nawe daima.
JIFUNZE KUENENDA KWA ROHO ILI USIMUHUZUNISHE ROHO MTAKATIFU
Shalom, hakuna namna mwamini anaweza kuishi maisha ya kumpendeza Mungu hapa duniani bila kuenenda au kuongozwa na Roho Mtakatifu kwani yeye ndiye aliyepewa jukumu la kutufundisha na kutuonyesha njia itupasayo kuiendea. Hivyo basi suala la kujifunza kuenenda kwa Roho ni la LAZIMA kwa kila mwamini ili aishi maisha aliyokusudiwa awapo duaniani na kuepuka matokeo ya kumhuzunisha Roho Mtakatifu maana gharama yake ni kubwa sana.
Biblia kwenye Waefeso 4:30 inasema ‘Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi’ na tena imeandikwa ‘Msimzimishe Roho’
(1Wathesalonike 5:19). Roho Mtakatifu ni Mungu, anayo nafsi ambapo ndani yake kuna hisia na kwa jinsi hiyo anaweza kufurahi au kuhuzunishwa pia (1Wathesalonike 5:6). Matokeo ya kumhuzunisha Roho Mtakatifu ni mabaya sana kwa mwanadamu na Mungu pia, ingawa mwenye kuathirika zaidi ni mwanadamu na ndio maana tunaonywa tusimuhuzunishe.
Kumhuzunisha Roho Mtakatifu ni kufanya au kusema jambo lolote lile ambalo litakatisha, kusimamisha au kuzuia kabisa utendaji au uongozi wake kwenye maisha yako. Naam kwa lugha nyingine kumuhuzunisha Roho Mtakatifu ni kumuwekea mpaka katika utendaji wake kwa kukataa uongozi, maonyo au ushauri wake unaolenga kuwezesha utekelezwaji wa kusudi la Mungu kupitia mwanadamu.
Je ni kwa namna gani mtu naweza kumhuzunisha Roho Mtakatifu?
Kwenye Isaya 63:9-10 imeandikwa ‘Katika mateso yao yote yeye aliteswa, na malaika wa uso wake akawaokoa; kwa mapenzi yake, na huruma zake, aliwakomboa mwenyewe; akawainua, AKAWACHUKUA siku zote za kale. Lakini WAKAASI, wakamhuzunisha Roho yake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia, akawa adui, akapigana nao’.
Matendo ya Mitume 7:51 inasema ‘Enyi wenye shingo ngumu, msiotahiriwa mioyo wala masikio, siku zote MNAMPINGA Roho Mtakatifu; kama baba zenu walivyofanya, na ninyi ni vivyo hivyo’. Pia Zaburi 78:40-41 inasema ‘Walimwasi jangwani mara ngapi? Na kumhuzunisha nyikani! Wakarudi nyuma wakamjaribu Mungu; WAKAMPA MPAKA Mtakatifu wa Israeli’ .
Maandiko haya yanatufanya tujue kwamba Roho Mtakatifu anaweza kuhuzunishwa kupitia UASI wa mwanadamu. Neno
uasi lina maana ya kupinga maelekezo au kukataa kuwa chini ya mamlaka au utawala wa Mungu na kwa jinsi hiyo ni kupingana na mamlaka husika. Kadri mtu anavyomwasi Mungu kwa njia yoyote ile ndivyo anavyomhuzunisha Roho Mtakatifu, naam ndivyo anavyotengeneza mpaka na hivyo kukata mawasiliano kati yao.
Uasi wa mwanadamu ni kikwazo au kizuizi kwa Roho Mtakatifu kumsaidia na kumuongoza katika mapenzi kamili ya Mungu. Ndio ile kusema ‘ siku zote mnampinga Roho Mtakatifu’ ( Matendo ya Mitume 7:51) ina maana kuna namna alitaka kuwasiaida, wao wakakataa usaidizi wake. Uasi unaweza kuwa kwenye neno la Mungu au maelekezo mahususi ambayo Roho Mtakatifu anampa mtu katika hatua mbalimbali za utendaji au utekelezaji wa kusudi la Mungu kwenye maisha yake.
Katika Zaburi 32:8 imeandikwa ‘Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama’ . Kwenye Yohana 14: 26 imeandikwa ‘Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia’ na Yohana 16:13 imeandikwa ‘Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake’.
Hii ni kutonyesha kwamba Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu amekusudia kuyaongoza maisha ya mwanandamu katika kusudi lake na hivyo mwanadamu hanabudi kuishi kwa kufuata uongozi wake. Sasa uasi mbaya zaidi ambao mwanandamu huufanya ni ule wa kutenda au kwenda kinyume na mapenzi au maelekezo ya Mungu kwenye maisha yake na kuamua kuyafanya yale yampendezayo yeye asijue kwamba ipo tofauti kubwa ya kiathari kati ya uasi unaohusisha mfumo rasmi wa utaratibu (procedure) na ule usiohusisha mfumo rasmi utaratibu (non-procedure).
Hebu tuone mifano kadhaa ndani ya Biblia – Dhambi ya Haruni na Miriam vs dhambi ya Haruni kutengeneza sanamu ya ndama (Hesabu 12:1-14, Kutoka 32:1-35). Pia uasi wa Ibrahimu na Sara (Mwanzo 16:1-6, Wagalatia 4:22-31). Pia unaweza ukajifunza jambo hili kupitia uasi wa Musa na Haruni (Hesabu 20:12, 27:14), Uasi wa Daudi (2Samweli 11:1-27), Uasi wa Sauli (1Samweli 15:1-35) nk.
Je upi ni ufumbuzi utakaomsaidia mwanadamu asimuhuzunishe Roho Mtakatifu? Ndugu zangu, kiwa matokeo na athari za uasi ni kubwa kiasi hicho kwa mwanadamu, basi ni lazima mwanadamu ajifunze kuenenda kwa Roho ili asimhuzunishe Roho Mtakatifu. Katika Wagalatia 5:16-18 imendikwa ‘Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria’.
Kuenenda kwa Roho maana yake kuishi kwa kuongozwa na utaratibu wa Roho Mtakatifu. Biblia katika Yeremia 31:33 inasema ‘ Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu’. Warumi 8:1-2 imeandikwa ‘Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti’ .
Zipo sheria kuu mbili zinazotaka kuongoza maisha na mwelekeo wa kila mtu dunaini. Moja ni sheria ya Roho wa uzima na ya pili ni sheria ya dhambi na mauti. Hizi ni sheria ambazo daima zinapingana na haziwezi kuja kupatana na hivyo ni uamuzi wa mwanadamu kuachagua sheria anayotaka iyaongoze maisha yake kwani mtu anapoishi kwa mojawapo ya sheria hizi sheria husika inamtenga mbali na sheria nyingine.
Kabla ya kifo cha Yesu msalabani, sheria ya dhambi na mauti inayofanya kazi kupitia mwili ilikuwa na nguvu dhidi ya torati (sheria). Torati ilikuwa ni dhaifu juu ya mwili na kwa hiyo maagizo (mahitaji) ya torati yasingeweza kutimizwa ndani ya mwanadamu. Hivyo Yesu alikuja ili aihukumu dhambi katika mwili wake, naam ili kwa njia hiyo wale waendao kwa Roho waweze kutimiza mahitaji ya sheria (Warumi 8:3-4).
Roho Mtakatifu anapokuwa ndani ya mtu kuna vitu (mafuta, hekima, nguvu, neema) anaachilia ndani au juu ya mtu husika ili kumsaidia namna ya kuenenda awapo duniani. Nasikitika kusema kwamba ‘bila kujifunza na kuwa na nidhamu ya kuenenda kwa Roho, waamini wataendelea kuwa watu wenye kulalamika kila siku huku wakipoteza fursa nyingi za mafanikio sambamba na kushindwa kuishi maisha ya ushindi hapa duniani’
(Wagalatia 5:18, Luka 4:18, 1Yohana 2:27).
Kumbuka Roho Mtakatifu anao utaratibu (sheria) ambao sharti tuujue na kuufuata ndipo tutaweza kutembea naye au kueneneda kwa Roho. Mtu anapochagua kuenenda kwa Roho, Roho Mtakatifu kutokana na nafasi yake wa wajibu wake kwetu atamuongoza mtu husika katika shauri sahihi. Naam, hata hivyo ili mtu aenende kwa Roho ni lazima; kwanza atambue nafasi ya Roho Mtakatifu (Yohana 14:17) , pili ampe kibali cha kuyaongoza maisha yake ( 1Petro 1:21) na mwisho ajue namna ya kuhusiana na kuwasiliana na Roho Mtakatifu.
Naam, nidhamu ya kujifunza na kudumu kuenenda kwa Roho itakusaidia usiseme au kufanya mambo unayotaka wewe wala kuyatafuta yakupendezayo, bali uishi sawasawa na mapenzi ya Mungu. Chagua leo kuenenda kwa Roho, nawe hutajutia maamuzi yako ya kuokoka bali ndivyo utakavyojua upendo na uweza wa Mungu katika kuwaongoza watoto wake kwenye shauri lake wawapo duniani.
Utukufu na heshima vina wewe Yesu, wastahili BWANA.

Ijumaa, 24 Agosti 2018
USIKATE TAMAA WALA USIVUNJIKE MOYO -YOUR RAINY SEASON IS COMING!
Nilipokuwa mdogo nilikuwa namuona MAMA akichambua maharage, alikuwa anaweka *maharage mazima* kwenye sufuria ya kupikia, na *maharage mabovu* alikuwa anayatoa kisha anayatupa mbali jalalani.!
Chakushangaza.. mvua ikinyesha maharage yale yale mabovu ndio yanakuwa ya kwanza kuota na kuchipua..
Yalitupwa yakiwa mabovu yasiyofaa.. lakini yanaota.. kisha yanatoa maharage mengine mazima na bora zaidi kuliko yalivyotupwa mwanzo yakiwa mabovu! “
Hii imenifanya nijifunze kuwa ni muda/wakati tu utakao amua hatma yako.. Pia jinsi Mungu anavyokuona ni tofauti kabisa na watu wanavyokuona..
Inawezekana ukaonwa/ukajiona kama maharage mabovu leo.. lakini hakika *mvua ya Mungu* ikikunyeshea UTAOTA na kuwa wa thamani na KUZAA/KUTENGENEZA WATU WENGINE BORA ZAIDI YA WEWE..
Inahitaji wakati tuu
Uvumilivu..
Na kujua kusudi la Mungu na mawazo ya Mungu ni tofauti na ya binadamu….
USIKATE TAMAA WALA USIVUNJIKE MOYO
YOUR RAINY SEASON IS COMING
Wewe ni bora na unafaa sana.!
Kila jambo chini ya jua lina wakati wake haijalishi jinsi ulivyo leo.
Mungu awabariki na nawatakia siku njema
BARIKIWA.
HIVI UNAJUA , MTU AACHI POMBE NDIO AOKOKE, BALI AOKOKE NDIPO AACHE POMBE?

Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi sana.
Duh! Hiyo kali kwa kweli…
Je hujawahi kusikia mtumishi akikemea watu au mtu aache pombe, kisha aokoke? Au binti akiambiwa “acha uhuni, uokoke leo. ” au hujawahi kuona mtu akilazimishwa aache kitu fulani ambacho kwa kweli ni chukizo kwa Mungu, ili aokoke! Sasa hivyo ndivyo watumishi wengi husema, na Wamesahau kwamba anayemwezesha mtu fulani kuacha dhambi au uovu ni Mungu. Kama kweli anayekuwezesha kuacha dhambi ni Mungu basi ni dhahiri kabisa unamwitaji kwanza Mungu kisha Mungu akuwezeshe kuacha dhambi. Unajua ukimuhubiria mrevi aache pombe kisha ndipo aje kwa Bwana mimi nataka nikwambie hawezi kuacha pombe na hakika utamkosa huyo mtu kwa sababu si yeye awezaye, bali Roho mtakatifu ndiye awezaye kufanya kazi hiyo isipokuwa mwenye dhambi aoneshe kuhitaji msaada huo ili asaidiwe.
Hata wewe usije ukajisifia kwamba umeacha uchafu wako uliokuwa ukifanya hapo mwanzo kwa sababu ni mjanja sana. Sio kweli! Bali pale ulipoamua ukaweka nia, Mungu akakusaidia katika hilo. Lakini ujue hata kitendo cha kufanya maamuzi hayo, Mungu alihusika sana. Kumbuka tunaokoka kwa neema kwa njia ya imani katika Kristo Yesu ( Waefeso 2:8). Kanisa la leo limewakosa watu wengi walio dhambini kwa mafundisho manyonge yanayofundishwa, na matokeo yake tumejikuta tukihubiriana sisi kwa sisi na sio kwa walio nje tuwalete kanisani. Naikumbuka ile sheria ya dini yangu ya zamani kabla ya kuokoka, kasheria kalikuwa ni kuwazuilia wadada / wanawake wowote atakaye vaa nguo fupi! .
Lakini wanaume waliachwa kwa sehemu kubwa lakini ikafika wakati na wanaume wakaandikiwa kwa wale watakaovaa vikaushi kwamba makwapa yao yakionekana watolewe nje! Ni kweli mavazi yanapaswa yawe ya heshima. Lakini sheria hizi ni za wanadamu wa dini. Sasa nikuulize kama mdada wa mataifa kakimbilia kanisani kwa Yesu,kaja jinsi alivyo akiwa na nguo fupi maana ndio maisha yake yalivyo, Je wewe wa kanisani umzuie? Ebu jijibu sasa swali hilo. Vipi ukimzuia je si sawa na kumwambia rudi huko huko kwenye mataifa? Sasa Je, unategemea kwanza abadilike ndipo aingie kanisani / kwa Yssu. Sasa ni nani wa kumbadilisha huyo ikiwa ametoka duniani na wewe u mtu wa kanisani, je unafikiri ukimwambia arudi duniani awe kwanza safi ndipo aende kwa Bwana, dunia itamvadilisha? Weeeh thubutu! Nani kakwambia kwamba anaweza kubadilika akiwa huko duniani!!!!!
Kumbe kinachotakiwa ni kanisa ndilo limbadilishe baada ya kumpokea jinsi alivyo kwa maana bila shaka hata wewe ulipokelewa jinsi ulivyokuwa, sasa iweje wewe leo uweke msimamo wa kumtaka eti mtu kwanza abadilike ndipo aokoke. Ikiwa kama mpaka mtu abadilike ndipo aokoke, basi kuokoka hakuna maana, kwa maana kuokoka ni kwa mwenye dhambi jinsi alivyo, kisha Roho atambadilisha hatua hadi hatua. Ifike wakati sasa tujitambue kwa kuwakaribisha makahaba, waabuduo sanamu n. k tuwahubirie, waokoke kisha Mungu atashughulika nao kwa kuacha mambo yao. Usifikiri mchezo kuacha jambo fulani ikiwa unalipenda, bila Mungu ni ngumu na kwa kweli haiwezekani na huo ndio ukweli wenyewe.
Wainjilisti wenzangu!
Ebu ifike wakati tuone kwamba kazi ya kumfanya mtu kuacha dhambi ni ya Mungu sio ya mwenye dhambi. Tukilijua hilo tutakuwa na ujasiri mkubwa wa kuhubiri kweli, kisha tutawapata wengi na wengi watakuja kwa Kristo. Ile elementi / tabia ya kumkemea mwenye dhambi kama ya ulevi kwa kumwambia “acha pombe nakwambia, kisha uje uokoke ” tuiche, bali tuwaambie kwamba Yesu anakupenda naye atakusaidia kuacha pombe, bali wewe njoo tu kwa Yesu uokoke.
Kwa msaada zaidi pamoja na maombezi nipigie sasa kwa namba zilizopo hapo juu.
Jumatano, 22 Agosti 2018
JE MTU AKIFA ATAKUA HAI TENA
Ayubu 14:13-14 “ Laiti ungenificha kuzimuni, Ukanilinda kwa siri, hata ghadhabu zako zitakapopita, Na kuniandikia muda ulioamriwa, na kunikumbuka! Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena? Mimi ningengoja siku zote za vita vyangu, Hata kufunguliwa kwangu kunifikilie.”
Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele
Leo hii wakristo wote nchini wanaungana na wakristo wengine duniani kote pamoja na wayahudi kuadhimisha sikukuu ya Pasaka, kukumbuka tukio la kusulubiwa, kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo kulikotokea miaka zaidi ya 2000 iliyopita, huku Wayahudi wakiadhimisha miaka zaidi ya 3000 Tangu walipoadhimisha Pasaka ya kwanza katika siku ya 15 ya mwezi wa Nisan kwa mujibu wa Kalenda ya kiyahudi Hapo walipookolewa kutoka Misri.
Miaka mingi sana kabla ya kufufuka kwa Yesu, mtumishi wa Mungu Ayubu aliwahi kuuliza swali la msingi sana katika maisha ya mwanadamu, swali hili ni moja ya miongoni mwa maswali ya kifalsafa, swali hili liliulizwa kutokana na hoja zilizotolewa na watu wenye hekima mbali mbali waliokuja kumtia moyo ayubu na kujiuliza swali kwanini wanadamu wanateseka, swali kuhusu mateso hata leo limekuwa ni swali kubwa sana lenye mjadala mkubwa sana katika imani mbalimbali
· Wahindu wanaamini mateso yanatokana na KARMA yaani kuishi kwa kutenda Mema wanaamini kama ukiishi vibaya utazaliwa kitu kibaya na utapata shida, na hivyo katika mzunguko wa maisha Mungu atakupa mabaya na utachelewa kufika NIRVANA yaani mbinguni kukaa na Mungu
· Wabudha wanaamini kuwa mateso yanatokana na tamaa, yaani kama mwanadamu ataishi mbali na tamaa atakuwa ameingia NIRVANA hata kama bado yuko Duniani, hivyo wao hujifunza kuridhika na kujikana na kuitesa miili yao
· Waislam wanaamini kuwa mateso ni matokeo ya Kudra za mwenyezi Mungu, yaani ni mapenzi ya Mungu kwa kadiri ya majaliwa yake
· Wayahudi waliamini kuwa mtu anaweza kupata mateso kama matokeo ya dhambi zake au za wazazi wake kutokana na Mungu alivyoahidi kushuhulika na kizazi hata ta tatu na nne cha wampendao au wanaomchukiza
· Wakristo swala kuhusu Mateso ni swala pana sana na linaweza kuwa na ufafanuzi mpana sana wa kwanini wanadamu wanateseka, hata hivyo Kiongozi mkuu wa wokovu wetu yaani Yesu alikamilishwa kwa njia ya mateso
Katika kitabu cha Ayubu ni wazi kuwa Ayubu pamoja na rafiki zake walikuwa wakijadili kuhusu Mateso na sio mateso ya kawaida bali mateso ya mtu aliyeishi kwa haki, Ayubu ambaye inasemekana kuwa aliihi maisha ya hali alikuwa anateseka sana na hakuwa amepata tiba, licha ya mali yake kuwa imetekekea, licha ya kuwa amepoteza watoto wake wote, pia alikuwa na majipu mabaya yaliyokuwa yakifumba na kufumbuka mwili mzima kutoka kichwani hata unyayoni, Ayubu na wenzake walikuwa wamejadili na kutafuta suluhu bila kupata ufumbuzi na hivyo Aybu alikuwa anatazamia kufa aliamini kuwa sasa hakuna tumaini lingine lililosalia zaidi ya kifo tu, ndipo Ayubu akauliza katika hali yakukata tamaa
Kwamba mbona miti ikikatwa shina lake huchipuka? Na maji ya bahari hupwa na kujaa ni kama inaonekana kuwa viumbe hivyo vina matumaini lakini sivyo ilivyo kwa mwanadamu, inaonekama kama mtu akifa ni mwisho wa kila kitu na hakuna matumaini ya kurejea tena, Ayubu anamwambia Mungu kwa kuwa siku za mwanadamu za kuishi ni chache na zimejaa taabu, ni afadhali angewaacha tu bila kupata mateso maana hawatakuwako tena, Hata hivyo Ayubu alikuwa na imani kuwa iko namna atamuona Mungu tu hata kama mwili wake utaharibiwa alikuwa na imani kuwa macho yake yatamuona tu
Ayubu 19: 25-27 “Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi. Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi, Lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu; Nami nitamwona mimi nafsi yangu, Na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine. Mtima wangu unazimia ndani yangu.”
Swali lililoulizwa na Ayubu Mungu aliwahi kumuuliza mtumishi wake Ezekiel katika namna nyingine,
Ezekiel 37:1-3 “. Mkono wa Bwana ulikuwa juu yangu, naye akanichukua nje katika roho ya Bwana, akaniweka chini, katikati ya bonde; nalo limejaa mifupa; akanipitisha karibu nayo pande zote; na tazama, palikuwa na mifupa mingi katika ule uwanda! Nayo, tazama, ilikuwa mikavu sana. Akaniambia, Mwanadamu, je! Mifupa hii yaweza kuishi? Nami nikajibu, Ee Bwana MUNGU, wajua wewe ”.
Wakati huu taifa la Yuda lilikuwa limechukuliwa utumwani Babel na kila kitu iimeaharibiwa na kufa hakukuwa na matumaini ya uhai tena ndio maana swali hili lilikuwa Gumu kwa Ezekiel yeye alijibu tu kuwa Bwana unajua wewe! Mtu awaye yote anapopitia katika mateso na huzuni na kukata tamaa huwa anafikiri kuhusu kurejeshwa tena katika hali aliyokuwa nayo mwanzoni your Golden Age!
Mtume Yohana ndiye mtume aliyeteseka sana kuliko mitume wote, inasemekana aliwahi kuviringishwa katika yasi na kuwashwa moto lakini alitoka akiwa safi, aliwahi kuchemshwa katika pipala mafuta ya lami lakini alitoka akiwa hai, alishuhudia wenzake na wakrito wengine wakifa na kuawa kwa kuliwa na simba kuchomwa moto na kadhalika yeye kutokana na kushindikana kufa waliamua kumpeleka katika kisiwa cha Patmo ili akateseke huko maisha yalikuwa ni yenye kuhuzunisha na kukatisha tamaa, Yesu alimuona Yohana akiwa amekata tamaa na alimpa ujumbe mkubwa wa kutia moyo
Yohana 1:17-18 “Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu .”
Swali la muhimu la kujiuliza ni kwanini Yesu alijitambulisha kuwa yu hai yaani amefufuka? Ni muhimu kufahamu kuwa ujumbe muhimu kwa mtu ANAYETESEKA, ALIYEKATA TAMAA , na ALIYE KATIKA HALI YA KUFA ni UJUMBE WA UFUFUO Yesu alifahamu kuwa huu ndio ujumbe pekee unaoweza kumpa mtu tumaini Jipya!
Habari njema kwa ndoa iliyokufa sio kuolewa tena ni kurejea tena kwa furaha iliyotoweka na upendo uliotoweka katika ndoa yake.
Tunapoisheherekea pasaka na kukumbuka kufufuka kwa Bwana wetu Yesu ni ujumbe wa matumaini
kwamba Bwana Yesu alikufa na akafufuka na kuwa mauti haimuwezi na kuwa ni yeye ndiye mwenye funguo za mauti na kuzimu, ki msingi Yesu anajibu la swali la Ayubu kuwa mtu akifa atakuwa hai tena Yesu anajibu swali hili kuwa ndio mtu akifa anaweza kuwa hai tena na anatutangazia wazi kuwa yeye anazofunguo za mauti na kuzimu na hivyo anauwezo wa kufufua matumaini yaliyotoweka kwako, anauwezo wa kufufua huduma yako, anauwezo wa kurejesha watoto wako, ana uwezo wa kurejesha kila kilicho haribiwa na kuuawa na ibilisi, ana uwezo wa kurejesha na kufufua taifa linalomtumaini yeye, Pasaka hii mimi sihitaji habari nyingine yoyote nahitaji kusikia habari za matumaini ya kuwa Yesu Kristo yuko hai na ndiye mwenye Mamlaka ya kifo na uzima na ana uwezo wa kufufua ndoto zetu, maisha yetu, matumaini yetu, uzima wetu, mimi sihitaji waraka wa maaskaofu nahitaji kumuona mteteaji wangu akisimama kiunitetea dhidi ya kila aina ya unyonge na utumwa Pasaka ina uhusiano na ukombozi nahitaji kumuoja Yesu akinikomboa mimi na familia yangu na watu wangu na taifa langu hii ndio habari njema ya ujasiri kuwa mauti haina nguvu katika maisha yetu, imepoteza mamlaka ni yesu pekee mwenye mamlaka hiyo yeye atafufuka pamoja na mashaka yangu yeye atahuisha nafsi yangu!

PEMBE YA WOKOVU NI NINI
Mstari wa Msingi: Zaburi 18:2-8 “Bwana ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na PEMBE YA WOKOVU wangu, na ngome yangu.
YQNitamwita Bwana astahiliye kusifiwa, Hivyo nitaokoka na adui zangu. Kamba za mauti zilinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu. Kamba za kuzimu zilinizunguka, Mitego ya mauti ikanikabili. Katika shida yangu nalimwita Bwana, Na kumlalamikia Mungu wangu. Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake, Kilio changu kikaingia masikioni mwake. Ndipo nchi iliyotikisika na kutetemeka, Misingi ya milima ikasuka-suka; Ikatikisika kwa sababu alikuwa na ghadhabu. Kukapanda moshi kutoka puani mwake, Moto ukatoka kinywani mwake ukala, Makaa yakawashwa nao.”
Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele viwili vifuatavyo:-
1. Maana ya neno Pembe
2. Maana ya pembe ya wokovu
Maana ya neno Pembe.
Neno Pembe ya wokovu limetajwa mara nytingi sana katika sehemu mbalimbali za Maandiko Matakatifu yaani Biblia, Lakini itakuwa muhimu zaidi kama tutafahamu kwa pamoja kwa kina na mapana na marefu maana ya Pembe ya wokovu, neno Pembe na uhusiano wake katika wokovu.
Neno Pembe katika Biblia waebrania wanaiita “ SHOFAR” imetumika katika maandiko kuelezea mambo mengi sana, katika namna nyepesi wote tunafahamu kuwa Pepmbe ni aina mfupa mgumu unaojitokeza na kukua katika kichwa cha mnyama, Mwanzo 22:13 , Pembe ya mnyama hususani kondoo mume inatumika kama silaha ya Kushambulia, Kulinda, kuonyesha mamlaka na utawala na kuleta Hofu, ni ishara ya nguvu, uweza na ushindi, kwa Msingi huo maandiko yanapotaja Pembe mara nyingi hutumika kuelezea uweza na nguvu.
Kwa lugha nyingine ya kinabii neno Pembe pia linatumika kuelezea kuhusu Serikali, au ufalme au nguvu ya dola yaani nguvu za ufalme huo unaweza kuona katika Daniel 7:7, 24 “ Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.; 24 Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu.” Unaweza kuona hivyo Pembe huzungumzia NGUVU au uweza wa KIJESHI Dolla, kwa msingi huo taifa au kabila fulani linapoondolewa ngvu zake lugha ya kibiblia maana yake pembe zake zimekatiliwa mbali Yeremia 48:25 “Pembe ya Moabu imekatika, na mkono wake umevunjika, asema Bwana. Mlevyeni; kwa maana alijitukuza juu ya Bwana ”
Pembe pia hutumika kuelegea nguvu ya Upako yaani uwezo wa Roho Mtakatifu,Pembe katika agano la kale zilitumika pia kuweka mafuta maalumu ya upako ambao wangepakwa watu kama makuhani, manabii na wafalme kwa kusudi la kutimiza mapenzi ya Mungu mfano 1. Samuel 16:1-3 “ Bwana akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israeli? Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakupeleka kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe. Samweli akasema, Nawezaje kwenda? Sauli akipata habari, ataniua. Basi Bwana akasema, Chukua ndama pamoja nawe, ukaseme, Nimekuja ili kumtolea Bwana dhabihu. Ukamwite Yese aje kwenye dhabihu, nami nitakuonyesha utakayotenda; nawe utamtia mafuta yule nitakayemtaja kwako, 13 Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na roho ya Bwana ikamjilia Daudi kwa nguvu tangu siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama .” Aidha Pembe zilitumika kama tarumbeta za kumsifu Mungu na zilipopulizwa pembe kwaajili ya utukufu wa Mungu ngome za adui zilianguka na kusambatratika kabisa Yoshua 6:1-5 “ Basi Yeriko ulikuwa umefungwa kabisa kwa sababu ya wana wa Israeli; hapana mtu aliyetoka wala hapana mtu aliyeingia. Bwana akamwambia Yoshua, Tazama, nimeutia Yeriko katika mkono wako, na mfalme wake, na mashujaa wake. Nanyi mtauzunguka mji huu, watu wote wa vita, mkiuzunguka mji mara moja. Fanya hivi siku sita. Na makuhani saba watachukua tarumbeta saba za pembe za kondoo waume, mbele ya hilo sanduku; na siku ya saba mtauzunguka mji mara saba, nao makuhani watapiga tarumbeta zao. Kisha itakuwa watakapopiga hizo pembe za kondoo waume kwa nguvu, nanyi mtakaposikia sauti ya tarumbeta, watu wote watapiga kelele kwa sauti kuu; na ukuta wa mji utaanguka chini pale pale, na hao watu watapanda, kila mtu akiendelea mbele kukabili. ”
Tafasiri nyingine ya kibiblia ilihusu pembe za madhabau kwa maana ya kuwa kila kona ya madhabau kulikuwa na pembe nne, pembe hizi zilivyunyiziwa damu wakati wa kutoa dhabihu ili kwamba watu waweze kufanyiwa upatanisho kwa mungu na kupata rehema, sehemu hii ya pembe pia ilitumika kwa ibada ya upatanisho kati ya Mungu na wanadamu Walawi 8:15 “ Kisha akamchinja; na Musa akaitwaa damu yake, akaitia katika pembe za madhabahu pande zote kwa kidole chake, akaitakasa madhabahu, kisha akaimwaga hiyo damu hapo chini ya madhabahu, na kuitakasa, ili afanye upatanisho kwa ajili yake.” Eneo hili la pembe za madhabahu lilitumika pia kumaanisha MAKIMBILIO au kujisalimisha endapo mtu angekuwa na tatizo linalohitaji kujihami, au kujitakia rehema hususani alipataka kuuawa 1Wafalme 1:50 “Adonia naye akaogopa mbele ya Sulemani; akaondoka, akaenda, akazishika pembe za madhabahu .” Kwa hivyo kimsingi hizo ndizo maana ya Pembe kibiblia.
Maana ya Pembe ya wokovu!
Kama tulivyoweza kuona kwa uapana na kina na urefu kuhusu maana ya neno Pembe sasa ni muhimu kwetu tukarejea katika andiko letu la Msingi Zaburi 18: 2 “ Bwana ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na PEMBE YA WOKOVU WANGU, na ngome yangu.” Hapo sasa utaweza kumuelewa vema mwandishi wa zaburi anapozungumzia kuhusu Pembe ya wokovu wake, kwamba ana maanisha nini, Pembe kwa msingi huo ilitumika kuelezea WOKOVU neno wokovu katika kiyunani ni SOTERIA ambalo maana yake ni Nguvu ya kuweka Huru, Nguvu ya kukuondoa Hatarini, Nguvu ya kukulinda na Hatari, Nguvu ya ukombozi, Nguvu ya kuharibu mipango ya adui, Nguvu ya kusambaratisha nguvu za adui yako Zaburi 75:10 “ Pembe zote za wasio haki nitazikata, Na pembe za mwenye haki zitainuka” Kazi hii ya ukombozi Israel walikuwa na ufahamu na Roho Mtakatifu aliwafunulia wazi kuwa Dola hii au nguvu au serikali hii inayoweza kuleta ukombozi, inayoweza kuvunja vunja nguvu za adui zako, inayoweza kuharibu kila aina ya nguvu za upinzani, inayoweza kukulinda, inayoweza kukuokoa, inayoweza kukupa rehema na neema, inayoweza kukutetea dhidi ya adui zako dhidi ya waliokudhulumu, dhidi ya waonevu, dhidi ya magonjwa, dhidi ya masononeko, dhidi ya ufisadi, dhidi ya fitina, faraka , masengenyo mateto kunenwa vibaya, kusingiziwa, kuvunja nuksi mikosi na balaa, kukuweka huru nguvu hii inaitwa PEMBE YA WOKOVU
LUKA 1:67-75 “. Na Zakaria, baba yake, akajazwa Roho Mtakatifu, akatabiri, akisema, Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, Kwa kuwa amewajia watu wake, na kuwakomboa. Ametusimamishia pembe ya wokovu Katika mlango wa Daudi, mtumishi wake. Kama alivyosema tangu mwanzo Kwa kinywa cha manabii wake watakatifu; Tuokolewe na adui zetu Na mikononi mwao wote wanaotuchukia; Ili kuwatendea rehema baba zetu, Na kulikumbuka agano lake takatifu; Uapo aliomwapia Ibrahimu, baba yetu, Ya kwamba atatujalia sisi, Tuokoke mikononi mwa adui zetu, Na kumwabudu pasipo hofu, Kwa utakatifu na kwa haki Mbele zake siku zetu zote .”(my god mya god ribasakarabashanda! Rebosokoroboshi ribabababaskataritoli yenderebekisha sanda) Zekaria akajazwa Roho Mtakatifu kwa msingi huo maneno hayo ni ya Roho Mtakatifu, Na hapo yanamtaja “ YESU KRISTO” ndni yake kuna ukombozi, ndani yake kuna kuokolewa na adui zetu ndani yake kuna kutolewa mikononi mwa wanaotuchukia Mungu wangu, kumbe kwaajili ya amani yetu na ulinzi wetu hatuhitaji pembe za waganga wa kienyeji, kwa sababu tunayo pembe tumesimamishiwa Pembe ya wokovu, Jina Yesu maana yake ni wokovu, Yesu ni mwenye nguvum kama zilivyo nguvu za Pembe za wanyama wakali, wenye nguvu Yuko mwenye nguvu kuliko vyote yeye ni pembe ya wokovu wangu, yeye ndio kimbilio letu yeye ndio mahali sahihi pa kujisalimisha mmmmmhmmmm my God najisikia kuhubiri hapa kuna mtu nasema naye hapa viti haviwezi kukalila maana nimempata Yesu, nimepata nguvu nina upako nina ulinzi wa ajabu sio kitu kingine ni Yesu mwana wa Mungu aliye hai pambe ya wokovu wangu!
Mungu akubariki tafadhali si mbaya ukinijuza jinsi ulivyobarikiwa na somo hili sms or whatsapp 0628080839

PESA KATIKA MDOMO WA SAMAKI
Andiko: Mathayo 17:24-27
“Hata walipofika Kapernaumu, wale watozao nusu-shekeli walimwendea Petro, wakasema, Je! Mwalimu wenu hatoi nusu-shekeli? Akasema, Hutoa. Naye alipoingia nyumbani, Yesu alitangulia kumwuliza, akisema, Waonaje, Simoni? Wafalme wa dunia hutwaa kodi ama ushuru kwa watu gani? Kwa wana wao au kwa wageni? Naye aliposema, Kwa wageni, Yesu alimwambia, Basi, kama ni hivyo, wana ni mahuru. Lakini tusije tukawakwaza, enenda baharini ukatupe ndoana, ukatwae samaki yule azukaye kwanza; na ukifumbua mdomo wake utaona shekeli ichukue hiyo ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako.”
Utangulizi:
Ni muhimu kufahamu kwamba hapa duniani, kila mtu anahitaji fedha kwaajili ya kutimiza mahitaji yake, Bila fedha wakati mwingine ni vigumu kukidhi mahitaji yetu yote,kwa kadiri siku zinavyokwenda na hali ya uchumi inabadilika na kwa sababu hiyo fedha inazidi kuwa ngumu sana, na maisha yanabadilika mno na kwa sababu hiyo fedha zinahitajika ili wana wa Mungu wasiweze kukudhalilisha, kutokana na kukosekana kwa fedha,
Yesu anatoa suluhu namna ya kupata fedha katika muujiza huu
Muujiza wa Yesu, kumtuma Petro kuvua samaki na kupata fedha unaonekana kutajwa katika Injili ya Mathayo pekee, penginepo kwa vile yeye alikuwa mtoza ushuru, ingawa watoza ushuru hawa hawakuwa mawakili ya serikali ya Rumi bali walikuwa watoza ushuru kwaajili ya ujenzi wa Hekalu.
Watoza ushuru wa Hekalu walimuuliza Petro kama Mwalimu nwao analipa kodi ya hekalu nae aliwajibu kuwa analipa,Petro aliporejea Yesu alizungumza naye kuhusu swala aliloulizwa kuhusu kodi
“Naye alipoingia nyumbani, Yesu alitangulia kumwuliza, akisema, Waonaje, Simoni? Wafalme wa dunia hutwaa kodi ama ushuru kwa watu gani? Kwa wana wao au kwa wageni? Naye aliposema, Kwa wageni, Yesu alimwambia, Basi, kama ni hivyo, wana ni mahuru .” Yesu alikuwa akimaanisha wao kama wana wa Mungu wako huru wasingelipaswa kulipa kodi ile, lakini ili aiwakwaze watoza ushuru, Yesu alitoa maagizo kwa Petro nini anapaswa kufanya ili kukidhi hitaji hilo la kulipa kodi, tunaona Yesu akimuelekeza Petro kwenda kutupa Ndoana na kuvua samaki na samaki yule wa Kwanza angekuwa na fedha ambayo ingetosha kulipa Kodi yake na Petro. Watu wengi na walimu wengi wa neno la Mungu hawasemi mengi kuhusu muujiza huu,
Lakini mimi naona yako mambo ya kujifunza katika muujiza huu
1. Wote tunahitaji fedha kwaajili ya kukidhi mahitaji mbalimbali tuliyonayo katika Maisha
2. Wote tunahitaji fedha kwaajili ya kumuabudu Mungu na kumtumikia
3. Wote tunahitaji fedha kwaajili ya kulipia ada za shule za vijana wetu
4. Wote tunahitaji fedha kwaajili ya hatima ya wale wanaotuzunguka na wanaotutegemea
5. Wote tunahitaji fedha kwaaji ya kujiwekea hadhina mbinguni, tunapomtolea yeye na kuwapa wajane na masikini, na kutunza wazee wetu, na kuukuza ufalme wa Mungu.
Kama Petro na Mwalimu wake hawangelipa Kodi hii wangedhalilika, watu wangemsema Yesu, kuwa anajifanya mtu wa Mungu lakini halipi kodi ya Hekalu, hivyo Yesu anatambua kuwa watoto wake wanapokosa fedha wanadhalilika, wanaingia katika fadhaa, na hivyo alimuelekeza Petro nini cha kufanya.
Yesu alifanya Muujiza huu kuonyesha kuwa ana nguvu dhidi ya Fedha, “Jesus Has power over money” Yeye anauwezo juu ya fedha, Tatizo kubwa la watu wengi wa Mungu leo hawajawahi kumuambia Yesu kuwa wanashida ya fedha, linapokuja tatizo la fedha haraka sana hapo ndipo watu wengi sana hutumia akili na kuanza kusugua vichwa vyao, sio tu kusugua vichwa pia huanza kuumia moyo, na kuingia hofu na hata kulalamika, Tumesahau kabisa kuwa Mungu wetu anauwezo wa kutusaidia kama alivyomfanyia Petro .
Ni muhimu kufahamu kuwa Yesu ana uwezo juu ya fedha, Biblia inaeleza wazi kuwa yeye ingawa alikuwa tajiri alifanyika Masikini ili sisi tuwe matajiri 2Wakoritho 8:9 “Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.”
Biblia inatufundisha kuwa ni yeye anayetupa nguvu ya kupata utajiri Kumbukumbu 8:18 “Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.”
Biblia inaonyesha kuwa Petro alikuwa na uhitaji na hivyo huenda alimtaarifu Yesu kilichotokea, kwa ufupi alimuomba, kuhusu uhitaji wa kulipa kodi kwamba wanadaiwa kodi, na Yesu alijibu maombi hayo, kwa msingi huo kama tunavyoomba kwaajili ya mahitaji mengine tunahitaji pia kumuomba Mungu atupe fedha ili tusidhalilike.
Biblia inasema Hamna kitu kwa sababu hamwombi ni lazima tumuombe Mungu kwaajili ya hali ya uchumi wa familia zetu na mahitaji yetu, Sala ya Bwana inasema utupe leo riziki yatu ya kila siku, riziki yetu ya kila siku haiwezi kupatikana bila kuhusisha fedha je tumewahi kuomba fedha?
labda wengi tumefungwa na ile dhana ya fundisho la shina la mabaya yote ni kupenda fedha, lakini biblia inamaanisha kupenda fedha kuliko Mungu, na haimaanishi kuwa watu wake hawahitaji fedha, hapa mimi nazungumzia ule uhitaji fedha wa kawaida, kama ilivyokuwa kwa Petro anadaiwa kodi, labda huenda na wewe unadaiwa kodi ya nyumba, ama una madeni, ama unadaiwa ada ya watoto wako na kadhalika haja za namna hii ni vema pia Mungu akazijua, wengi hunijia wakitaka maombezi ya namna mbalimbali, lakini sijawahi ona mtu akinijia kuomba maombi apate fedha, wengi linapokuja swala la uhitaji wa kifedha, wanatumia akili zao wenyewe na wanaishia kupata msongo wa mawazo, huku haja hiyo ikiwa haijawasilishwa kwa Mungu, kutokumwambia Mungu uhitaji wetu wa kifedha ni daharau, ni sawa na kufikiri kuwa labda swala la kupata fedha Mungu haliwezi, lakini maandiko yanasemaje yote yawezekana kwa Mungu. kwa nini unasumbuka hali neno la Mungu linasema
Wafilipi 4: 6 maandiko yanasema “ Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.”
Je umewahi kumuomba Mungu waziwazi kwamba akupatie fedha ? umewahi kumuombea Mumeo, mkeo, wazazi, ndugu zako wawe na upenyo wa kifedha? Lazima tumuombe Mungu katika hitaji hili.
Mathayo 7: 7-11 Biblia inatukumbusha kuwa, Mungu ni Baba mwenye upendo ambaye huwapa watoto wake Mahitaji kwa kadri walivyoomba.
Anauliza je ni nani kati yenu mwanaye akiomba mkate atampa Jiwe? Au akiomba samaki atampa nyoka? Nauliza umewahi kumuomba Mungu akupe fedha ? au umetamani tu kuwa na fedha kwa kutumia akili zako mwenyewe bila kumwambia Mungu
Anamalizia kwa kusema " kama ninyi mlio waovu mwaweza kuwapa watoto wenu vipawa vyema je si zaidi sana Baba yenu Wa Mbinguni .........'' Hivyo kile tunachokiomba ndicho tutakachopokea.
1 Petro 5: 7 maandio yanasema wazi kuwa, Mungu hujishughulisha Zaidi na Mambo Yetu na hivyo tumpe yeye Fadhaa/haja zetu.
Anasema.
7 huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.
Kama utasema hujui namna ya kuomba hususani kuomba fedha kwa Mungu basi fuata muongozo wa mambo ya kuombea:-
Mambo ya kuombea:
• Omba Mungu akuweke mbali na Madeni, Yesu na Petro hapa walikuwa wanadaiwa kodi ya hekalu. na petro alipatwa na fadhaa
• Omba Mungu akusaidie usiwe mzigo kwa wazazi wako
• Omba Mungu kwamba akupe fedha nyingi kuliko matumizi
• Omba Mungu kwamba uwe na uwezo wa kukopesha na sio kukopa
• Vunja roho ya umasikini, kataa mikosi inayoendana na kipato chako
• Kataa roho ya umasikini na magonjwa na masumbufu
• Kemea Roho za wizi, hasara, mikosi, chuma ulete, kukopera na jicho baya, Mwambie Mungu akupatie ulinzi wa kutoshja katika mali zako.
Mwambie Mungu atumie ujuzi aliokupa au atakaokupa kukupa fedha
Yesu alitumia ujuzi aliokuwa nao Petro, kumpatia fedha, Petro alikuwa Mvuvi kabla ya kumtumikia Mungu, kwa kuwa mwanafunzi wa Yesu. Hivyo Yesu alitumia ujuzi na kipawa alichokuwa nacho ili kupata fedha ya kulipa kodi. alimuagiza aende akavue samaki na muujiza ulikuwa ndani ya samaki wa kwanza atakayevuliwa, kumbe fedha zetu ziko katika midomo ya samaki, ni lazima twende kwenye ujuzi ule tulionao tuweze kuzitoa fedha zetu huko na kukidhi mahitaji yetu tuliyo nayo
Fanya kazi kwa bidii, ile kazi aliyokupa Mungu fanya kwa uaminifu, fanya kama unamtumikia Mungu yeye anasema atazibariki kazi za mikono yako.
Yesu hakumwambia Petro akacheze Biko wala tatu mzuka hii ni michezo ya watu waliokata tamaa, wanaishi kwa kubahatisha, ni michezo ya watu masikini, wanaoishi kwa ndoto za mchana, wakitarajia kitu kutoka kwa miungu ya bahati nasibu, Mungu hajatuleta duniani ili tuishi maisha ya kubahatisha kanuni kuu za mafanikio ziko katika kazi naujuzi au kipawa ulichopewa na Mungu huko ndioko pesa yako iliko,
Biblia inatutaka tufanye kazi kwa bidii, Pesa iko katika mdomo wa samaki. Lakini ni lazima ukavue, ukienda kuvua samaki yule utakayemvua ana pesa mdomoni mwake, za kukidhi mahitaji yako ya ya jamaa zako, Nikutakie uwajibikaji mwema na Mungu aibariki kazi ya mikono yako Amen. Nakukumbusha kuwa fedha yako iko katika midomo ya samaki endenda ukatupe ndoana.

BWANA YU KARIBU NA WALIOVUNJIKA MOYO, NA WALIOPONDEKA ROHO HUWAOKOA.
Andiko la msingi: Zaburi 34:17-19 “ Walilia, naye Bwana akasikia, Akawaponya na taabu zao zote. Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, Na waliopondeka roho huwaokoa. Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini Bwana humponya nayo yote.”
"Bwana yu Karibu na Waliovunjika Moyo, Na waliopondeka Roho Huwaokoa Zaburi 34:18"
Utangulizi:
Ni muhimu kufahamu kuwa tuwapo duniani wanadamu tunazungukwa na changamoto nyingi, kwa kawaida Mungu ameruhusu tuweze kupitia nchangamoto za aina mbalimbali kwa makusudi mbalimbali, aidha ya kutufundisha ama kutufanya tukue kiroho, kihekima na kimaadili lakini wakati mwingine kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe, hata hivyo wakati tunapopitia changamoto hizo, mara kadhaa wanadamu huwa tunakata tamaa, na tunaweza kujiuliza kama hivi Mungu anaona kweli? Hivi Mungu yupo? Kama yupo kwa nini anaachia jambo kama hili, kwa nini hakuzuia, kwa nini hakunitahadharisha mapema? Mbona yuko kimya Hivi yeye yupo kweli?tunaweza kufikiri kuwa Mungu ametuacha.
Katika nyakati hizi ngumu ndio nyakati ambazo ni rahisi kumuwazia Mungu kwa upumbavu, yaani kumfikiria Mungu kwa namna isiyofaa,Watakatifu waliotutangulia waliokuwa na ujuzi kuhusu Mungu walifahamu kuwa wanadamu wana changamoto nyingi maandi yanasema hivi kupitia Ayubu;-
Ayubu 14: 1 “Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. ”
Wote tunafahamu jinsi Ayubu alivyopitia majaribu na mateso Magumu lakini Biblia inatuambia kuwa Ayubu katika dhiki yake hakuwahi kumkufuru Mungu wala kumuwazia Mungu kwa upumbavu,
Ayubu 1:20-22 “ Ndipo Ayubu akainuka, akalirarua joho lake, kisha akanyoa kichwa chake, na kuanguka chini, na kusujudia; akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana na libarikiwe. Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu .”
Hali kama hii ndio iliyomtokea mwandishi wa Zaburi hii, kwa mujibu wa masimulizi ya tamaduni za kiyahudi Zaburi hii imethibitika kuwa iliandikwa na Daudi, au moja ya viongozi wa kwaya wa Daudi, na mazingira ya uandishi wa zaburi hii ulitokana na tukio la Daudi kunusurika katika hatari mbaya iliyokuwa ikimkabili, Zaburi hii iliandikwa mara baada au kwa kusudi la kukumbuka namna Daudi alivyonusurika katika hatari ngumu katikati ya mfalme wa wafilisti alipokuwa akitafutwa na Sauli ili aweze kuuawa Katika Mazingira haya magumu Daudi aliweza kujifanya mwendawazimu ili kupata namna ya kuondoka mikononi kwa Akishi mfalme wa wafilisti.
1Samuel 21:10-15 “Basi Daudi akaondoka, akakimbia siku ile, kwa hofu ya Sauli, akamwendea Akishi, mfalme wa Gathi. Nao watumishi wa Akishi wakamwambia, Je! Huyu siye yule Daudi, mfalme wa nchi? Je! Hawakuimbiana habari zake katika ngoma zao, kusema,Sauli amewaua elfu zake,Na Daudi makumi elfu yake. Naye Daudi akayatia maneno hayo moyoni mwake, akamwogopa sana Akishi, mfalme wa Gathi. Akaubadilisha mwenendo wake mbele yao, akajifanya mwenye wazimu mikononi mwao, akakuna-kuna katika mbao za mlango, na kuyaacha mate yake kuanguka juu ya ndevu zake. Ndipo huyo Akishi akawaambia watumishi wake, Angalieni, mwaona ya kuwa mtu huyu ana wazimu; basi, maana yake nini kumleta kwangu? Je! Mimi nina haja ya watu wenye wazimu, hata mmemleta kiumbe hiki ili aonyeshe wazimu wake machoni pangu? Je! Huyu ataingia nyumbani mwangu? ”
Ni katima Mazingira ya aina hii ndio Daudi alipoimba zaburi hii ya 34 akzizungumza maneno ya kushangaza sana hata baada ya tukio hili gumu namna hii Daudi aliweza kumsifu Mungu, alionyesha kuwa Mungu ni tumaini lake, hakutaka kulalamika alitaka watu wote wawe wanyenyekevu wamtumaini Mungu wamweleze shida zao na kuwa yeye atawaitikia kwa kuwa Ni Mungu aliye karibu na watu wake angalia maneno yake hiyo isiyo ndefu sana Zaburi 34:1-22
1. Nitamhimidi Bwana kila wakati, Sifa zake zi kinywani mwangu daima.
2. Katika Bwana nafsi yangu itajisifu, Wanyenyekevu wasikie wakafurahi.
3. Mtukuzeni Bwana pamoja nami, Na tuliadhimishe jina lake pamoja.
4. Nalimtafuta Bwana akanijibu, Akaniponya na hofu zangu zote.
5. Wakamwelekea macho wakatiwa nuru, Wala nyuso zao hazitaona haya.
6. Maskini huyu aliita, Bwana akasikia, Akamwokoa na taabu zake zote.
7. Malaika wa Bwana hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.
8. Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini.
9. Mcheni Bwana, enyi watakatifu wake, Yaani, wamchao hawahitaji kitu.
10. Wana-simba hutindikiwa, huona njaa; Bali wamtafutao Bwana hawatahitaji kitu cho chote kilicho chema.
11. Njoni, enyi wana, mnisikilize, Nami nitawafundisha kumcha Bwana.
12. Ni nani mtu yule apendezwaye na uzima, Apendaye siku nyingi apate kuona mema?
13. Uuzuie ulimi wako na mabaya, Na midomo yako na kusema hila.
14. Uache mabaya ukatende mema, Utafute amani ukaifuatie.
15. Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake hukielekea kilio chao.
16. Uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya, Aliondoe kumbukumbu lao duniani.
17. Walilia, naye Bwana akasikia, Akawaponya na taabu zao zote.
18. Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, Na waliopondeka roho huwaokoa.
19. Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini Bwana humponya nayo yote.
20. Huihifadhi mifupa yake yote, Haukuvunjika hata mmoja.
21. Uovu utamwua asiye haki, Nao wamchukiao mwenye haki watahukumiwa.
22. Bwana huzikomboa nafsi za watumishi wake, Wala hawatahukumiwa wote wamkimbiliao.
Unaweza kuona hatupaswi kukata tamaa wala kuvunjika Moyo katika mazingira yoyote, katika hali Ngumu zinazotukabili Mungu na aendelee kuwa Mungu wetu, tusimuwazie kwa Upumbavu tuendelee kuuona mkono wake, na kumtegemea yeye katika hali zozote, tusinungunike, bali afadhali kumlilia yeye,
Manunguniko yanaondoa Baraka za Mungu, Manunguniko, yanamkasirisha sana Mungu, badala ya kulalamika na kunung’unika ni afadhali kumlilia yeye na kumhimidi yeye Daudi anasema atamhimidi Bwana kila wakati maana yake katika hali yoyote na Mungu yu Karibu na waliovunjika moyo na wanaonyenyekea kwake yeye huwakomboa huwahurumia na kuitikia kilio chao.
Mungu aitikie kilio chako Ndugu yangu, Mungu na awe karibu nawe Mungu asikupungukie Mungu asikufanye ukufuru Usivunjike moyo, wakati unapopita katika Magumu, Mungu yuko Karibu, Mungu hajatutupa wala hajakutupa wewe anakujali yuko Karibu nawe mtafute wakati huu wa dhiki yako atakutokea nawe utasadiki ya kuwa Mungu amenituma nikuhakikishie kuwa Yuko Karibu nawe Bila shaka atakufuta Machozi yako leo, BWANA YU KARIBU NA WALIOVUNJIKA MOYO, NA WALIOPONDEKA ROHO HUWAOKOA.
FURAHA TIMILIFU
Mstari wa Msingi: Yohana 16: 23 -24 “ Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; FURAHA YENU IWE TIMILIFU .”
Je wewe hutegemea hali ya nje kama chanzo cha Furaha maishani mwako? Angalia kwamba Mungu ndio chanzo kikubwa cha furaha timilifu na sio vinginevyo
Utangulizi:
Maisha ya mwanadamu yanategemea sana kuwa na furaha ili yawe maisha, na mwanadamu siku zote anafanya kila kitu kwaajili ya furaha yake tuu. Furaha ndio kilele cha maisha ya mwanadamu, kila analolifanya mwanadamu lengo lake kuu ni kupata furaha.
Mathalani ukitoa msaada kwa mtu moyo huwa na furaha, ukipongezwa au kusifiwa kwa jambo fulani moyo huwa na furaha, ukiwa mshika ibada moyo huwa na furaha, ukiwa na mke mwema au mume mwema moyo huwa na furaha vilevile, ukiwa na watoto wazuri na wenye adabu na kujiheshimu, ukifanya kazi kwa ufanisi, ukipata malipo ya kazi yako au mshahara moyo huwa na furaha kadhalika, ukisikiliza mziki au filam ama picha na hata kusoma vitabu moyo huwa na furaha pia, Ukiwa na mafanikio makubwa, ukijenga nyumba, ukiwa na mashamba, ukinunua gari, ukipandishwa cheo, ukichumbiwa, ukiolewa, ukizaa mtoto, ukiwa na afya njema moyo huwa na furaha, ukipewa tuzo, ukishinda uchaguzi, ukimiliki kampuni na kufanikiwa Moyo huwa na furaha Lakini pamoja na hayo yooote bado utaweza kuona kuwa hakuna furaha iliyo timilifu, Je ni wapi tunaweza kuona na kuwa na furaha timilifu?
Furaha nini?
Ni vigumu sana kuielezea furaha zaidi ya neno lenyewe furaha, Katika kiingereza neno linalotumika kuelezea furaha ni “ JOY ” ambalo katika lugha ya kiyunani ni “ CHARA ” linatamkwa “KHA-RAH ” ambalo maana yake ni Hali ya kujaa raha katika nafsi kutokana na kufikia au kufanikiwa katika jambo fulani, hali ya kuwa na raha isiyo na mipaka kutokana na kutoshelezwa kwa nafsi.
Katika imani ya Kikristo tunaweza kusema ni Raha ya nafsi ndani ya mwamini anayopipata kama matokeo ya Neema na upendo wa Roho Mtakatifu kumuwezesha mtu huyo, kufurahia kuwa na uhusiano na Mungu na kumjua Yesu Kristo, Neno lake na makusudi yake na tumaini lililo ndani yake.
Je ni watu wangapi wana furaha?
Ukiulizwa swali je una furaha je unaweza kulijibu vipi? Ni swali gumu sana, kwani unaweza ukawa una furaha lakini unafahamu kuwa furaha hiyo haidumu milele. Labda una furaha kutokana na kuwa una familia nzuri, lakini kwa kina utaona kuwa furaha hiyo inategemea uwepo wa familia nzuri, na uwepo huo ukitenganishwa kwa vifo, maisha, mabadiliko mbalimbali basi furaha yake nayo inaisha. Hivyo kuna furaha za milele na furaha ya muda mfupi.
Kila mtu anapenda kuwa na furaha, na lengo kuu la maisha ni kuwa na furaha. Hata hivyo furaha ya watu wengi sana sio furaha timilifu kwa sababu furaha zao zinatawaliwa na hali ya nje ya maisha yao angalia mfano huu:-
Mtu moja alikuwa anamiliki nyumba nzuri sana ni nyumba ya thamani na ilikuwa yenye kupendeza na yenye mvuto mkubwa sana katika mji aliokuwa anaishi, na jamaa huyu aliipenda nyumba yake sana watu wengi waliwahi kumuendea na kumuomba awauzie hata kwa bei kubwa mara mbili ya thamani yake lakini alikataa, wakati fulani bwana huyu alisafiri na aliporejea aliikuta nyumba yake ikiwa inawaka moto mkubwa sana na hivyo alipatwa na huzuni kubwa mno! Mamia ya watu walikusanyika kwaajili ya kuangalia namna ya kusaidia kuuzima moto ule, lakini hakuna walichofanikiwa kukiokoa katika moto ule
Mara mwanae mkubwa alimjia na kumnongoneza sikioni, Baba usiogope, “Niliiuza nyumba hii jana na niliiuza kwa bei nzuri sana, bei ilikuwa nzuri kiasi ambacho nisingeliweza kukusubiri au kukutaarifu, Hivyo unisamehe bure tu baba”
Baba yule alivuta pumzi na kuzishusha akimshukuru Mungu kwani sasa amekuwa moja ya washuhudiaji wa ajali ile kama walivyo wengine,
Mara mwanae wa pili alikuja mbio akimkimbilia na kumbwambia baba unafanya nini uangalia nyumba yetu ikiwa inaungua? Baba alimjibu kijana yule kuwa tulia kwani kaka yako aliiuza tayari kwa bei nzuri, Kija ayule alimwambia baba yake kuwa tulichukua kiwango fulani tu cha fedha na sio zote hivyo nina mashaka kama yule aliyenunua atakubali kumalizia ilihali nyumba imeungua!
Yule baba alianza kulia tena, machozi ambayo mwanzoni alikuwa ameshasahau,Moyo wake ulianza kwenda mbio sana na nguvu zikaanza kumuishia alikuwa mwenye huzini kubwa sana, Mara mtoto wake wa tatu akaja na kumwambie Baba yule mtu aliyenunua nyumba yetu ni mtu mwema na mwaminifu na mwenye kutunza sana ahadi kwani nimetoka kuongea naye sasa na ameniambia “ Haijalishi kwamba nyumba imeungua au la Nyumba ni yangu na nitalipa kiwango chote cha fedha tulichopatana, kwa kuwa hakuna aliyejua kuwa nyumba itaungua, Kisha wote wakasimama wakiwa wametulia kama washuhudiaji wengine wakiangalia nyumba inayoungua bila wasiwasi wowote!
Tunajifunza nini kutokana na kisa hiki? Watu wengi sana wanajisikia kuwa wenye furaha kutokana na hali ya nje ya mambo na sio ya ndani na kwa sababu hiyo hawawezi kuwa na furaha ya kweli, furaha ya kibinadamu ya ya dunia hii ni yenye kuyumba kutokana na hali halisi ya kubadilika badilika kwa mambo, aidha furaha ya kweli haipatikani kwa kuwakosea wengine.
Wako watu wengine wanafikiri kuwa watakuwa wenye furaha kwa sababu ya kukandamiza wengine, kuwatesa, kuwatendea vibaya, kuwashitaki, kuwasengenya, na kuwakosea ni muhimu kufahamu kuwa watu wote wanahitaji furaha kwa sababu hiyo kama huwezi kuwasaidia wengine kuwa wenye furaha basi jitahidi usiwe sababu ya huzuni zao, furaha ya kweli hua kwa kuhakikisha kuwa wengine wana furaha kama wewe na sio kuwakosea.
Faida za kuwa na furaha timilifu
Kwa mujibu wa wataalamu wa maswala ya saikolojia wanaeleza kuwa furaha ina faida kubwa sana
Zikiwemo
a. Inakulinda na magonjwa ya Moyo
b. Inaimarisha kinga za mwili
c. Inatupilia nje mikandamizo ya mawazo katika maisha
d. Inakulinda dhidi ya Magonjwa
e. Inarefusha maisha
Kitaalamu hata utungiswaji wa Mimba hutokea siku ambayo wana ndoa wote wamefurahi
Unawezaje kuwa na Furaha timilifu?
Kaa katika uwepo wa Mungu Zaburi 16:11 “Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya milele.” Unaweza kuona maneno Mbele za uso wako ziko furaha tele yanamaanisha mbele za uwepo wa Mungu “ Presence” kuna furaha tele, Musa alikuwa ni mtu aliyependa kukaa katika uwepo wa Mungu, alikaa uweponi mwa Munngu kiasi ambacho hakusikia njaa kwa siku 40 na hata aliporejea uso wake ulikuwa unangaa’ kiasi ambacho watu walishindwa kumtazama Kutoka 34:29-35 “ Hata ikawa, Musa aliposhuka katika mlima Sinai, na zile mbao mbili za ushuhuda zilikuwa mkononi mwa Musa, hapo aliposhuka katika mlima, Musa hakujua ya kuwa ngozi ya uso wake iling'aa kwa sababu amesema naye. Basi Haruni na wana wote wa Israeli walipomwona Musa, tazama, ngozi ya uso wake iling'aa; nao wakaogopa kumkaribia. Musa akawaita; Haruni na wakuu wote wa kusanyiko wakarudi kwake; Musa akasema nao. Baadaye wana wa Israeli wote wakakaribia; akawausia maneno yote ambayo BWANA amemwambia katika mlima Sinai. Na Musa alipokuwa amekwisha kusema nao, akatia utaji juu ya uso wake. Lakini desturi ya Musa ilikuwa alipoingia mbele za BWANA kusema naye, kuuvua huo utaji mpaka atoke; akatoka akawaambia wana wa Israeli maneno yote aliyoambiwa. Wana wa Israeli wakauona uso wa Musa ya kuwa ngozi ya uso wake Musa iling'aa; naye Musa akautia utaji juu ya uso wake tena, hata alipoingia kusema naye.”
Usitawaliwe na hali ya nje.
Habakuki 3:17-18 “ Maana mtini hautachanua maua, Wala mizabibuni hamtakuwa na matunda; Taabu ya mzeituni itakuwa bure, Na mashamba hayatatoa chakula; Zizini hamtakuwa na kundi, Wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng'ombe; Walakini nitamfurahia Bwana Nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu.” Kwa mujibu wa Habakuki ni kuwa yeye atamfurahi Mungu bila kujali kuwa mtini haujachanua maua, au zabibu hazina matunda aku mzaituni haukuzaa au mashamba hayakutoa chakula au mazizi mifugo kutokuwa na kitu, Yeye bado atafurahi, hii ni wazi kuwa Mungu ndio chanzo cha furaha yetu na sio vinginevyo.
Dumu katika kuomba.
Kwa mujibu wa Yesu Kristo ukweli ni kuwa maombi yanasaidia kwa kiwango kikubwa sana kuketa firaha timilifu, kila amtu anapaswa kuomba, maombi ni muhimu sana, usiache kuomba Yohana 16: 23 -24 “Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; FURAHA YENU IWE TIMILIFU .”
Mwamini Mungu na Kumtegemea.
Warumi 15:13 “Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu. ”, Imani katika Mungu na kumtegemea yeye kunaweza kutupa furaha timilifu.
Watumikie wengine Watu wanaowatumikia wengine huwa na furaha sana Duniani.
Na Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima.

Jumanne, 21 Agosti 2018
KUFUFUKA KWA YESU
KUFUFUKA KWA YESU.
=Yesu baada ya kukaa kwenye uso wa nchi huku akishughulika kuhakikisha wokovu unapatikana kwa watu wote watakao mwamini kama tulivyoona baadhi ya mambo muhimu Yesu aliyoyafanya kwenye ulimwengu wa roho, hatimaye siku ya tatu alifufuka.
=iyo tu kwamba alifufuka lakini yuko hai milele na milele na mauti haina nguvu juu yake tena,
=Yesu ni mwanadamu pekee hadi leo ambaye kaburi lake liko wazi, kwa sababu kama ni kufufuka tu siyo hoja, kuna watu wengi katika historia walifufuka lakini baada ya muda walikufa tena.
=Kufufuka kwa Yesu kuna umuhimu gani kwetu?
=Siwezi kwa leo nikaelezea mambo yote yaliyotokea ya ajabu kwa sababu ya Yesu kufufuka, lakini labda nikuoneshe kitu hapa;
=Kwanza kabisa imani yetu ina nguvu sana kwa sababu Yesu japo alikufa lakini alifufuka na akawa hai milele na milele.
=Yaani kama Yesu asingalifufuka imani yetu ingekuwa bure na asingekuwa na utofauti na waanzilishi wa dini zilizopo hapa duniani tunazozifahamu kama Muhamedi wa dini ya kiislamu na wengineo ambao hata sasa bado wamelala makaburini.
=Hebu angalia hii:
1Wakor 15;14 *“tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure”
Isitoshe hapo chini kwa msisitizo ikarudiwa;*

1Wakor 15;17 ” Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu”
=Yesu alipofufuka ni nini kilitokea?
=Jambo kubwa sana lilitokea kiroho kwa sababu kwa kufufuka kwake aliishinda mauti ambayo ndiyo ilikuwa inafanya kazi kwenye maisha ya mwanadamu kwa sababu ya dhambi.
=Tena mauti ninayoiongelea hapa ni mauti ya kiroho ambayo ni kutengwa na Mungu milele.
=Kwa hiyo mwili wake ulifanyika limbuko (mzaliwa wa kwanza) kwa ajili ya wote wanaomwamini Yesu kwa hata wakipatwa na mauti ya kimwili lakini bado watafufuliwa tena na kuvikwa miili ya mbinguni na waishi milele na milele kama mwokozi wao.
1Wakor 15:20-23 “Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala. Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu. Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa. Lakini kila mmoja mahali pake; limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja”
=Kama unakumbuka tuliona kwamba Yesu pia anaitwa mzaliwa wa kwanza wa waliyokufa, ikimaanisha kwamba yeye ndiye mtangulizi kwa ajili ya wengi waliyokufa katika yeye kwamba siku moja nao watafufuka kama yeye.
=Hebu angalia tena hapa;
1Wakor 15:55-57 “Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako? Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati. Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo”

=Kuna mambo mengi sana hapa ya kujifunza na ninajua tutaendelea kuyaona zaidi, lakini kwa sasa angalau uwe na haya maarifa na taarifa hizi zikusaidie kujua mambo yaliyotendeka siku ulipookoka na wewe ambaye hujaokoka bado Bwana ana haja nawe tafadhali kama ukiwa tayari nione inbox au mwone mtumishi yeyote wa Mungu unayemwamini akusaidie.
KAZI YA YESU YA WOKOVU.
=Mungu wangu aendelee kukubariki sana kwa kuendelea kuwa mfuatiliaji mzuri wa masomo haya ambayo bado tunayo safari nzuri tu ya kuendelea kujifunza siri hizi za ufalme wa Mungu.
=Bado tupo kwenye eneo hili la kazi ya Yesu ya wokovu, tukiwa mwishoni mwishoni kabisa ninaamini Bwana ni mwema kwa ajili yetu anachotaka tukijue safari hii lazima tukipate hakika.
=Kipindi kilichopita tulipata nafasi ya kuangalia eneo kidogo tu kuhusu kifo cha Yesu, kwamba kwanini ilibidi kiwe cha msalaba na sii vinginevyo.
=Leo nataka tuangalie kuzikwa kwake na kukaa kaburini siku tatu na mwishowe kufufuka, kuna siri kubwa hapo.
*KUZIKWA KWAKE.*
=Kimsingi siongelei kile kitendo cha kuzikwa bali ninaongelea ule muda tangu aisalimu roho yake hadi alipofufuka siku ya tatu kama alivyosema.
=Kwanza kabisa niweke sawa hapa, Yesu hakukata roho bali aliitoa/aliisalimu roho yake, kwa maana kwamba Yesu kwa sababu ni Mungu hakuna mwanadamu ambaye angeweza kumwondoa uhai wake lakini alikubali mwenyewe kuutoa kisha akaja kuurudisha tena.
=Japo ukisoma kwenye tafsiri yetu ya Kiswahili injili ya Marko na Luka waliandika kwamba alikata Roho, lakini ukienda kwenye tafsiri za awali za biblia ya King James old version inasema wazi kwamba aliitoa roho yake na siyo kukata Roho.
=Injili ya mathayo na Yohana yenyewe ilitafisiriwa vizuri hilo neno; Mathayo alitimia neno kutoa uhai, la Yohana ametumia neno kuisalimu Roho, ambazo zote hizo zimekaa vizuri kama tafsiri za awali zilivyo.
=Hebu angalia hapa;
Yoh 10:17-18 *“Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena. Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu”*
=Ninaamini tuko sawa mpaka hapo.
=Sasa kilitokea nini katika ulimwengu wa roho wakati Yesu akiwa amekufa?
#Kwanza kabisa, kuanzia saa sita hadi saa tisa kabla Yesu hajaitoa roho yake kulikuwa na giza nchi yote maandiko yanasema hivyo; hiyo ilikuwa ni ishara kama ulimwengu wa giza umeshinda lakini dakika chache baadaye baada ya Yesu kuitoa Roho yake wakatu huo huo;
@tetemeko kubwa likatokea juu ya nchi,
@miamba ikapasuka,
@pazia la hekelu likapasuka kuoka juu hadi chini
@na cha kushangaza zaidi miili ya watakatifu wa kale waliyokuwa wamekufa wakafufuka tena wakawatokea wengi huko Yerusalemu.
=Hebu angalia maandiko;
Mathayo 27:50-53 *“Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake. Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka; makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala; nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi”*
=Siwezi nikaelezea kila kitu lakini nimelenga zaidi kwenye pazia kupasuka la kupaingia patakatifu hadi patakatifu pa patatakatifu, hapa ilikuwa inaonyesha sasa kwamba njia iko wazi kwa kila mmoja atakayeoshwa nah ii damu ya Yesu kuingia patakatifu kwa sababu naye ni kuhani.
=Lakini pia ilionesha kwamba Yesu aliye kuhani mkuu aliingia na damu yake mwenyewe hadi patakatifu pa patakatifu na kuinyunyizia kwenye kiti cha rehema ili kufanya upatanisho wa Mungu na manadamu wote watakao mpokea.
Haya yalifanyika ndani ya hizi siku tatu Yesu akiwa kwenye uso wa nchi kama maandiko yasemavyo;
2Wakor 5:19 *yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho.*
=Kuna kitu kingine cha ajabu hapa; mwanzoni kabla Yesu hajafa watu wote waliyokuwa wanakufa walikuwa wanaenda sehemu moja iliyokuwa imetenganishwa iliyoitwa kuzimu ambayo hadi sasa kuzimu ipo na ndiyo makao ya shetani na roho zote ovu pamoja na roho za wanadamu waliyokufa katika dhambi.
=Kabla ya Yesu ilikuwa kwamba ukifa mcha Mungu unaenda mahali palipoitwa kifuani mwa Ibrahimu ambako hakuna mateso badala yake ni raha tu, kulikuwa na shimo kubwa lililowatenga ambapo upande wa pili ndipo kuzimu kwenyewe ambako roho za wenye dhambi huenda kuteseka wakisubiri hukumu ya mwisho.
=Ndiyo maana kama unakumbuka Yesu alitoa mfano wa Tajiri na Lazaro namna walivyoishi duniani na maisha yao baada ya haya ya duniani.
=Sina muda lakini naomba usome kwa utulivu LUKA 16:19-31, *utakutana na kisa hiki. Ndiyo hali halisi ilivyokuwa kabla ya Yesu hajafa.*
=Ni nini kilitokea Yesu alipokufa?
=Tumesoma hapo kwamba miili ya watakatifu iliinuka kutoka makaburini tena hata hao waliyofufuka wakawatokea watu na kuuingia mji mtakatifu yaani Yerusalemu.
=Yesu naye alipokufa kama mwanadamu wa kawaida roho yake ilishuka kuzimu, na alipofika kuzimu kwenye eneo la wenye haki au watakatifu kama naye alivyokuwa mtakatifu akawatoa wote kuzimu ili awahamishie makao yao, ndiyo maana biblia inasema ilifufuka miili ya watakatifu peke yao.
=Ndiyo akaihamishia mahali pengine paitwapo paradiso ambapo ni juu wala siyo mbinguni lakini ni mahali pa raha ambapo watakatifu wanapokufa wanaishi hapo wakisubiria kufunuliwa kwa Yesu mara ya pili.
=Ndipo akaenda upande wa pili wa kuzimu ambapo ndipo makao ya shatani na roho za wanadamu waatenda dhambi waliyokufa ambako pia kuzimu maana yake ni kifungoni, na Yesu akaenda kuwahubiria huko siyo ili waokoke bali akawaeleza kwamba yeye ndiye aliyekuwa anahubiriwa na manabii na torati.
=Najua unashangaa hii hujawahi kuishikia lakini nakufundisha biblia, hebu angalia hii;
1Petro 3:18-20 *“Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa, ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni (kuzimu), akawahubiri; watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji”*
=Lakini baada ya hapo akamfuata Shetani ndipo akamnyang’anya ufunguo wa mauti na kuzimu, ikimaanisha sasa mauti haina nguvu wala kuzimu kwa wale wote wanaomwamini Yesu.
=Hizi ni siri za ndani kabisa ningeweza kukueleza mengi zaidi lakini Bwana atatupa wakati mwingine kuyachambua haya, hii nimekupa ili ikupe ujasiri na kujijua nafasi yako ilivyo ya thamani katika Kristo Yesu wewe uliyeokoka na kama bado nakupa nafasi kabisa unifuate inbox nitakuongoza vyema tena nitakuwa tayari kukusimamie hadi ukuo kiroho.
Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako. (KUM. 22:5 SUV).

Nimeonelea niongelee kidogo hili andiko ambalo sisi wahubiri tunalitumia sana kuwahukumu nalo wanawake katika uvaaji wao na kuwafanya wajisikie hatia sana.
Ili kuweza kulitafsiri andiko kiusahihi kwa ajili ya nyakati zetu lazima kwanza tujue linasema nini na lilikuwa lina maana gani kwa nyakati ambazo liliandikwa.
Anasema wazi mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume na mwanamume asivae mavazi ya mwanamke.
Hili andiko halisemi kuwa mwanamke asivae mavazi yanayofanana na ya mwanamume.
Katika siku za andiko hili mavazi ya wanaume na ya wanawake yalikuwa yanafanana kwa sehemu.
Ya kiume yalikuwa yanajulikana kama kanzu au joho wakati ya mwanamke yalikuwa yanajulikana kama gauni.
Wanaume na wanawake walikuwa wanafunga vitambaa vichwani mwao lakini namna ambavyo wanaume walifunga ilikuwa ni tofauti na vile wanawake walivyokuwa wanafunga.
Kuchukua hili andiko na kudhani linamaanisha wanawake wasivae suruali na kaptura ni kutokuelewa kabisa hili andiko linasema nini.
Mashati ya kike yanaitwa blauzi na blauzi za kiume zinaitwa shati.
Kuna mavazi ya aina nyingi tu katika tamaduni mbalimbali ambazo za kiume na za kike zinafanana.
Mtu wa Mungu kuna suruali za kike na za kiume.
Kuna kaptura za kike na za kiume.
Tofauti yake ni katika namna zilivyoshonwa.
Mwanamke anapaswa kuvaa mavazi ya kumsitiri na ajiepushe kuvaa mavazi ya kikahaba ndicho mimi ninachoona katika maandiko.
Mwanamke anaweza akavaa sketi au gauni na bado vikawa havijamsitiri na akawa amevaa kaptura au suruali na zikawa zimemsitiri.
Wadogo zangu wanaishi katika nchi ambayo vazi la heshima la kiume ni sketi.
Ukishaona unachohubiri hakiwezi kufaa kwenye kila jamii ya wanadamu jua tu kuwa unachohubiri kiko na shida mahali.
Hakuna mahali katika maandiko ambapo mwanamke amekatazwa kuvaa suruali au kaptura.
Kwanza wakati wa maandiko haya mavazi hayakuwepo.
Cha muhimu hapa ni sisi kama watu waliyookoka tuwe na kiasi katika namna tunavyovaa.
Tusivae huku tukiwa tumeacha sehemu zetu nyeti wazi au tukiwa tumebana mpaka kuchora viungo vyetu nyeti bila kujali tumevaa mavazi gani maana wakati mwingine mdada anaweza akavaa suruali ambayo haijambana wala kumchora na mwingine akavaa sketi au gauni iliyombana na ambayo haijamsitiri lakini yule aliyevaa suruali akaonekana kakosea katika kuvaa.
Ukifundisha mtu kuwa suruali ni kwa mwanamke ni dhambi akaenda India akakuta suruali ni vazi la heshima kwa mwanamke unamjengea ndani yake kuwaza kusiko sahihi kuwa wahindi wote wanakosea katika kuvaa.
Ukimfundisha mtu kuvaa sketi ni dhambi kwa mwanamume akienda Scotland na kukuta vazi la heshima la mwanamume wa kiScotish ni sketi utamjengea namna isiyo sahihi ya kufikiri kuwa waScotish wote ni wadhambi.
Tujiepushe kufundisha mitazamo yetu tubaki tunalihubiri neno.
Mtu anayesema kuwa suruali ni vazi la kiume ameamua kuwa finyu sana katika mtazamo wake anataka kutulazimisha wote tuwe finyu katika kuwaza kwetu.
Huyu mtu atafika mahali ambapo watu wapo huru kuvaa suruali bila ya kujali jinsia na atauhukumu wokovu wao based on mavazi bila ya kuzingatia maudhui na maana hasa ya maandiko anayotumia.
Tuache kutiana hatia kwa mitazamo yetu binafsi isiyo na uhusiano wowote na Neno la Mungu.
NI HIVYO TU YAANI.
Jisajili kwenye:
Maoni (Atom)
Machapisho Maarufu
|
|