💐🌺🏒🌾🌴🌴KESHA LA ASUBUHI LEO SEPTEMBER 14/2018🌻🌻🌷⛅🌴ISAYA🌾🌾

💐🌺🏒🌾🌴🌴KESHA LA ASUBUHI LEO SEPTEMBER 14/2018🌻🌻🌷⛅🌴ISAYA🌾🌾


Naye akaniambia, Enenda, ukawaambie watu hawa, Fulizeni kusikia, lakini msifahamu; fulizeni kutazama, lakini msione. Uunoneshe moyo wa watu hawa, ukayatie uzito masikio yao, ukayafumbe macho yao; wasije wakaona kwa macho yao, na kusikia kwa masikio yao, na kufahamu kwa mioyo yao, na kurejea na kuponywa. Isaya 6:9, 10.


K
azi ya Nabii huyu ilikuwa dhahiri; alipaswa kuinua sauti yake dhidi ya maovu yaliyoenea. Lakini aliogopa kutekeleza kazi hii pasipo kupewa uhakikisho wa tumaini. “Ee Bwana, hata lini?” (Isaya 6:11) aliuliza. Je asiwepo ye yote miongoni mwa wateule wako atakayeelewa, na kutubu, apate kuponywa?

Mzigo wa roho yake kwa niaba ya Yuda wanaopotoka haukubebwa bure. Utume wake usingelikosa kabisa matunda. Lakini bado maovu ambayo yalikuwa yakiongezeka kwa vizazi vingi yasingeondolewa katika siku zake. Katika maisha yake yote anapaswa kuwa mwalimu jasiri, mwenye uvumilivu-nabii wa matumaini pia wa hukumu. Kusudi la Mungu litakapotimilizwa hatimaye, matunda kamili ya juhudi zake, na ya kazi za wajumbe waaminifu wote wa Mungu, yataonekana. Masalia yataokolewa. Ili kwamba hili lipate kutokea, ujumbe wa onyo na kusihi ulipaswa kutolewa kwa waasi, Bwana alitamka, “Hata miji itakapokuwa ukiwa, haina wenyeji, na nyumba zitakapokuwa hazina watu, na nchi hii itakapokuwa ganjo kabisa; hata Bwana atakapowahamisha watu waende mbali sana, na mahame yatakapokuwa mengi ndani ya nchi” (aya 11, 12).

Hukumu nzito zilikuwa ziwaangukie wasiotubu hawa-vita, uhamisho, ukandamizaji, kupoteza mamlaka na heshima miongoni mwa mataifa-haya yote yalikuwa yaje ili kwamba wale ambao wangetambua ndani yake mkono wa Mungu waliyemkosea wapate kuongozwa kutubu. Makabila kumi ya kaskazini yalikaribia kutawanywa miongoni mwa mataifa, na miji yao kuachwa ukiwa; hata Yerusalemu hatimaye ilikuwa ianguke, na Yuda ilikuwa ichukuliwe mateka kwenda nje; hata hivyo bado Nchi ya Ahadi haikupaswa kubaki ikiwa imetupwa milele. -Review and Herald, March 11, 1915. 🌿🌿🍀BARIKIWENI

Maoni