MOJA: Maombi yanaimarisha uhusiano wa mtu na Mungu; Maombi ni mawasiliano baina ya mwanadamu na Mungu au ni njia ambayo tunaweza kuwasiliana na Mungu. Naamini unafahamu kuwa mawasiliano yanaongeza uhusiano wa mtu na mtu, hata wewe ni shahidi katika hili unaweza ukawa na ndugu wengi sana au marafiki wengi sana lakini yule ambaye anawasiliana na wewe mara kwa mara huyo ndiye anayeukuza ukaribu baina yenu kuliko wengine.
Ukweli wa mambo ni kwamba uhusiano wa mtu na mtu unaanzishwa kwa mawasiliano na vile vile unaweza ukapungua au hata ukafa kabisa kwa kukosa mawasiliano ya mara kwa mara. Mawasiliano ndio yanayofanya mahusiano yawe hai na yenye afya na ndio yanayowafanya watu wengi kuwa karibu. Tunapokuwa tunaomba mara kwa mara uhusiano wetu na Mungu unakuwa kwa kasi sana kuzidi yule asiyeomba, au yule anayeomba mara moja moja au yule anayeomba kwa viwango vya juu zaidi. Na kama tujuavyo, kadiri uhusiano wa mtu na mtu unavyokuwa na kuongekezeka ndivyo wanavyoweza kushirikishana mambo mengi zaidi.
MBILI; Maombi yanaweza kubadili maamuzi ya Mungu aliyoyapanga kwa taifa au kwa mtu ili afanye sawa sawa na vile wewe unataka lakini sawa sawa na kusudi lake; “Siku hizo Hezekia akaugua, akawa katika hatari ya kufa. Isaya, nabii, mwana wa Amozi, akamjia akamwambia, Bwana asema hivi, Tengeza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona. Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana akasema, Nakusihi, Bwana, ukumbuke sasa, jinsi nilivyokwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana. Ikawa, kabla Isaya hajatoka katika mji wa kati, neno la Bwana likamjia, kusema, Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, Bwana, Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama, nitakuponya; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa Bwana.” (2 FAL. 20:1-5). Hezekia alijua aljua na aliamini kuwa maombi yanaweza kubadili maamuzi ya Mungu la sivyo asingeomba. Soma pia Yona 3:1-10.
Kama maombi yanaweza kumshawishi Mungu kubadilisha maamuzi basi maombi yanaweza kutumika kubadilisha maamuzi ya mtu, ipo mifano mingi ya kibiblia inayoelezea juu ya maamuzi ya wanadamu yaliyobadilishwa baada ya maombi, hapo juu nimezungumzia tu mifano ya maombi yaliyobadilisha maamuzi ya Mungu. Maombi yanaweza kugeuza maamuzi ya yule bosi wako pale kazini, maombi yanaweza yakabadili maamuzi ya watawala. Maombi yanaweza kubadili matamko na laana za ukoo, inawezekana familia inapitia kwenye vifungo vya umaskini mkubwa pamoja na kufanya kazi kwa juhudi, roho za magonjwa, vifungo vya kutokuoa au kutokuolewa, kwa njia ya maombi mwamini anaweza kubadili laana zote na kuwa Baraka.
TATU: Maombi yanatupa nguvu ya kutoingia majaribuni ; Yesu aliwawaambia wanafunzi wake maneno haya kwa uzito sana baada ya kuona wanafunzi hawana maisha ya maombi! Walikuwa wanafikiri jukumu la kuomba ni la Yesu tu! Kama sisi tunavyofikiri sasa, kwamba jukumu la kuomba ni la watu fulani tu, na si la kwetu.
Kila mahali ambapo Yesu alikuwa anaomba wanafunzi wake ambao leo tunawatambua kama mitume! Walikuwa hawana maisha ya maombi. Angalia hapa Luka 9:28-32, “Baada ya maneno hayo yapata saa nane, akawatwaa Petro na Yohana na Yakobo, akapanda mlimani ili kuomba (Hilo ndio lilikuwa lengo lakini angalia matokeo yake).Ikawa katika kusali kwake sura ya uso wake ikageuka…” (Hapa Yesu anaomba peke yake wale aliopanda nao walishamwacha walikuwa na usingizi). Petro na wale waliokuwa pamoja naye walikuwa wamelemewa na usingizi: lakini walipokwisha amka…”
Inaonyesha wazi walikuwa wamelala wakati Yesu anaomba! Walikuwa wanaona shida kuomba kama sisi tunavyoona shida! Lakini tatizo lilikuwa linajirudia tena na tena kwa wanafunzi mpaka ikabidi Yesu awaambie madhara ya kutokuwa na maisha ya maombi! Hapa lilikuwa tukio jingine sio lile la mlimani! Mathayo 26:40-41, “Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, je! Hamkuweza kukesha nami hata saa moja? Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni.
NNE; Maombi yanaondoa vikwazo au vipingamizi vyote: “Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.” (Marko 11:23-24).
TANO; Maombi hugeuza mioyo na tabia ya watu wengine; “Ndipo mfalme akaniambia, Una haja gani unayotaka kuniomba? Basi nikamwomba Mungu wa mbinguni. Nikamwambia mfalme, Mfalme akiona vema, na ikiwa mimi, mtumishi wako, nimepata kibali machoni pako, tafadhali unipeleke mpaka Yuda, niuendee mji wa makaburi ya baba zangu, nipate kuujenga. Mfalme akaniuliza, (malkia naye ameketi karibu naye), Safari yako itakuwa ya siku ngapi? Nawe utarudi lini? Hivyo mfalme akaona vema kunipeleka; nami nikampa muda. Tena nikamwambia mfalme, Mfalme akiona vema, na nipewe nyaraka kwa maliwali walio ng'ambo ya Mto, ili waniache kupita mpaka nifike Yuda; nipewe na waraka kwa Asafu, mwenye kuutunza mwitu wa mfalme, ili anipe miti ya kufanyizia boriti kwa malango ya ngome ya nyumba, na kwa ukuta wa mji; na kwa nyumba ile nitakayoingia mimi. Naye mfalme akanipa, kama mkono mwema wa Mungu wangu ulivyokuwa juu yangu.” (Nehemia 2:4-8).
SITA; Maombi ni njia ya uponyaji wa kimwili na kiroho; “Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana. Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa.” (Yakobo 5:14-15).
SABA; Maombi huleta msukumo wa kiroho na kumtia mtu nguvu wakati mtu fulani anapokabiliwa na hali ya kushindwa: “Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni; mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu; mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha; (Wakolosai 1:9-11).
NANE; Maombi hufungua milango ya nguvu za Mungu zisizo za kawaida katika maisha yetu: Maombi yanaachilia mwaliko kwa Mungu wetu kutenda kazi katika ulimwengu wetu. Kwa ujumla, maombi ni njia ya kuita nguvu ya Kimungu ili ikatende kazi katika eneo kusudiwa. “Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa.”(MDO 16:25-26)
TISA; Maombi ni njia Mungu aliyoichagua kuzuia nguvu na utendaji kazi wa shetani duniani; “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho… kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote (EFES. 6:12, 18)
KUMI; Kwa njia ya maombi unaweza kuwa mahali kiroho ambapo huwezi kuwa kimwili: Kwa njia ya Maombi unaweza ukasafiri mapaka mkoa mwingine na ukaenda kufanya shughuli za kihuduma huko.
KUMI NA MOJA; Maombi yanakuwezesha kushiriki maamuzi mbali mbali pamoja na Mungu kwenye ulimwengu wa roho: Lakini ndugu yangu nikuambie ukweli maombi ni njia nzuri sana ambayo unashiriki moja kwa moja maamuzi ya mambo mengi katika jamii unayoishi. Inawezekana ni katika familia, au kanisani, au kama ni mtaani kwako, kama ni katika nchi yako na kadhalika. Mungu ametuweka kama mawakili katika maeneo yetu tulipo. Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya; wala msimwache akae kimya, mpaka atakapoufanya imara Yerusalemu, na kuufanya kuwa sifa duniani.”(ISA. 62:6-7)
WARUMI 8:28, " Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. "
KUMI NA MBILI; Kwa maombi yako ingia katika ulimwengu wa roho ili ubadili hali ya ulimwengu wa kimwili: Ulimwengu wa roho ndio mkuu zaidi kuliko ulimwengu wa mwili. Ulimwengu wa roho ndio unautawala ulimwengu wa mwili. Dunia na vyote vyenye kuonekana vimetokea kutokana na ulimwengu ule usioonekana. kila jambo linalotekea katika ulimwengu wa mwili limeanzia katika ulimwengu wa roho. Kufaulu na kushindwa kwetu kote, kabla ya kudhihirika katika ulimwengu wa mwili, kuna kuwa kumepangwa na kutekelezwa katika ulimwengu wa roho. Biblia inasema; “mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo” (3 YOH. 1:2). Hii inamaanisha kwamba mafanikio yetu ya kweli kimwili yanategemea mafanikio yetu ya kiroho. Ni katika ulimwengu wa roho ndiko tunakosimama au kuanguka, tunakoshinda au kushindwa. Adui akitaka kukudhibiti, anamdhibiti roho yako, ukishindwa kufanikiwa rohoni, huwezi kufanikiwa mwilini.

Maoni
Chapisha Maoni