HIVI UNAJUA , MTU AACHI POMBE NDIO AOKOKE, BALI AOKOKE NDIPO AACHE POMBE?
Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi sana.
Duh! Hiyo kali kwa kweli…
Je hujawahi kusikia mtumishi akikemea watu au mtu aache pombe, kisha aokoke? Au binti akiambiwa “acha uhuni, uokoke leo. ” au hujawahi kuona mtu akilazimishwa aache kitu fulani ambacho kwa kweli ni chukizo kwa Mungu, ili aokoke! Sasa hivyo ndivyo watumishi wengi husema, na Wamesahau kwamba anayemwezesha mtu fulani kuacha dhambi au uovu ni Mungu. Kama kweli anayekuwezesha kuacha dhambi ni Mungu basi ni dhahiri kabisa unamwitaji kwanza Mungu kisha Mungu akuwezeshe kuacha dhambi. Unajua ukimuhubiria mrevi aache pombe kisha ndipo aje kwa Bwana mimi nataka nikwambie hawezi kuacha pombe na hakika utamkosa huyo mtu kwa sababu si yeye awezaye, bali Roho mtakatifu ndiye awezaye kufanya kazi hiyo isipokuwa mwenye dhambi aoneshe kuhitaji msaada huo ili asaidiwe.
Hata wewe usije ukajisifia kwamba umeacha uchafu wako uliokuwa ukifanya hapo mwanzo kwa sababu ni mjanja sana. Sio kweli! Bali pale ulipoamua ukaweka nia, Mungu akakusaidia katika hilo. Lakini ujue hata kitendo cha kufanya maamuzi hayo, Mungu alihusika sana. Kumbuka tunaokoka kwa neema kwa njia ya imani katika Kristo Yesu ( Waefeso 2:8). Kanisa la leo limewakosa watu wengi walio dhambini kwa mafundisho manyonge yanayofundishwa, na matokeo yake tumejikuta tukihubiriana sisi kwa sisi na sio kwa walio nje tuwalete kanisani. Naikumbuka ile sheria ya dini yangu ya zamani kabla ya kuokoka, kasheria kalikuwa ni kuwazuilia wadada / wanawake wowote atakaye vaa nguo fupi! .
Lakini wanaume waliachwa kwa sehemu kubwa lakini ikafika wakati na wanaume wakaandikiwa kwa wale watakaovaa vikaushi kwamba makwapa yao yakionekana watolewe nje! Ni kweli mavazi yanapaswa yawe ya heshima. Lakini sheria hizi ni za wanadamu wa dini. Sasa nikuulize kama mdada wa mataifa kakimbilia kanisani kwa Yesu,kaja jinsi alivyo akiwa na nguo fupi maana ndio maisha yake yalivyo, Je wewe wa kanisani umzuie? Ebu jijibu sasa swali hilo. Vipi ukimzuia je si sawa na kumwambia rudi huko huko kwenye mataifa? Sasa Je, unategemea kwanza abadilike ndipo aingie kanisani / kwa Yssu. Sasa ni nani wa kumbadilisha huyo ikiwa ametoka duniani na wewe u mtu wa kanisani, je unafikiri ukimwambia arudi duniani awe kwanza safi ndipo aende kwa Bwana, dunia itamvadilisha? Weeeh thubutu! Nani kakwambia kwamba anaweza kubadilika akiwa huko duniani!!!!!
Kumbe kinachotakiwa ni kanisa ndilo limbadilishe baada ya kumpokea jinsi alivyo kwa maana bila shaka hata wewe ulipokelewa jinsi ulivyokuwa, sasa iweje wewe leo uweke msimamo wa kumtaka eti mtu kwanza abadilike ndipo aokoke. Ikiwa kama mpaka mtu abadilike ndipo aokoke, basi kuokoka hakuna maana, kwa maana kuokoka ni kwa mwenye dhambi jinsi alivyo, kisha Roho atambadilisha hatua hadi hatua. Ifike wakati sasa tujitambue kwa kuwakaribisha makahaba, waabuduo sanamu n. k tuwahubirie, waokoke kisha Mungu atashughulika nao kwa kuacha mambo yao. Usifikiri mchezo kuacha jambo fulani ikiwa unalipenda, bila Mungu ni ngumu na kwa kweli haiwezekani na huo ndio ukweli wenyewe.
Wainjilisti wenzangu!
Ebu ifike wakati tuone kwamba kazi ya kumfanya mtu kuacha dhambi ni ya Mungu sio ya mwenye dhambi. Tukilijua hilo tutakuwa na ujasiri mkubwa wa kuhubiri kweli, kisha tutawapata wengi na wengi watakuja kwa Kristo. Ile elementi / tabia ya kumkemea mwenye dhambi kama ya ulevi kwa kumwambia “acha pombe nakwambia, kisha uje uokoke ” tuiche, bali tuwaambie kwamba Yesu anakupenda naye atakusaidia kuacha pombe, bali wewe njoo tu kwa Yesu uokoke.
Kwa msaada zaidi pamoja na maombezi nipigie sasa kwa namba zilizopo hapo juu.
Maoni
Chapisha Maoni