Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako. (KUM. 22:5 SUV).


Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako. (KUM. 22:5 SUV).

Nimeonelea niongelee kidogo hili andiko ambalo sisi wahubiri tunalitumia sana kuwahukumu nalo wanawake katika uvaaji wao na kuwafanya wajisikie hatia sana.
Ili kuweza kulitafsiri andiko kiusahihi kwa ajili ya nyakati zetu lazima kwanza tujue linasema nini na lilikuwa lina maana gani kwa nyakati ambazo liliandikwa.
Anasema wazi mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume na mwanamume asivae mavazi ya mwanamke.
Hili andiko halisemi kuwa mwanamke asivae mavazi yanayofanana na ya mwanamume.
Katika siku za andiko hili mavazi ya wanaume na ya wanawake yalikuwa yanafanana kwa sehemu.
Ya kiume yalikuwa yanajulikana kama kanzu au joho wakati ya mwanamke yalikuwa yanajulikana kama gauni.
Wanaume na wanawake walikuwa wanafunga vitambaa vichwani mwao lakini namna ambavyo wanaume walifunga ilikuwa ni tofauti na vile wanawake walivyokuwa wanafunga.
Kuchukua hili andiko na kudhani linamaanisha wanawake wasivae suruali na kaptura ni kutokuelewa kabisa hili andiko linasema nini.
Mashati ya kike yanaitwa blauzi na blauzi za kiume zinaitwa shati.
Kuna mavazi ya aina nyingi tu katika tamaduni mbalimbali ambazo za kiume na za kike zinafanana.
Mtu wa Mungu kuna suruali za kike na za kiume.
Kuna kaptura za kike na za kiume.
Tofauti yake ni katika namna zilivyoshonwa.
Mwanamke anapaswa kuvaa mavazi ya kumsitiri na ajiepushe kuvaa mavazi ya kikahaba ndicho mimi ninachoona katika maandiko.
Mwanamke anaweza akavaa sketi au gauni na bado vikawa havijamsitiri na akawa amevaa kaptura au suruali na zikawa zimemsitiri.
Wadogo zangu wanaishi katika nchi ambayo vazi la heshima la kiume ni sketi.
Ukishaona unachohubiri hakiwezi kufaa kwenye kila jamii ya wanadamu jua tu kuwa unachohubiri kiko na shida mahali.
Hakuna mahali katika maandiko ambapo mwanamke amekatazwa kuvaa suruali au kaptura.
Kwanza wakati wa maandiko haya mavazi hayakuwepo.
Cha muhimu hapa ni sisi kama watu waliyookoka tuwe na kiasi katika namna tunavyovaa.
Tusivae huku tukiwa tumeacha sehemu zetu nyeti wazi au tukiwa tumebana mpaka kuchora viungo vyetu nyeti bila kujali tumevaa mavazi gani maana wakati mwingine mdada anaweza akavaa suruali ambayo haijambana wala kumchora na mwingine akavaa sketi au gauni iliyombana na ambayo haijamsitiri lakini yule aliyevaa suruali akaonekana kakosea katika kuvaa.
Ukifundisha mtu kuwa suruali ni kwa mwanamke ni dhambi akaenda India akakuta suruali ni vazi la heshima kwa mwanamke unamjengea ndani yake kuwaza kusiko sahihi kuwa wahindi wote wanakosea katika kuvaa.
Ukimfundisha mtu kuvaa sketi ni dhambi kwa mwanamume akienda Scotland na kukuta vazi la heshima la mwanamume wa kiScotish ni sketi utamjengea namna isiyo sahihi ya kufikiri kuwa waScotish wote ni wadhambi.
Tujiepushe kufundisha mitazamo yetu tubaki tunalihubiri neno.
Mtu anayesema kuwa suruali ni vazi la kiume ameamua kuwa finyu sana katika mtazamo wake anataka kutulazimisha wote tuwe finyu katika kuwaza kwetu.
Huyu mtu atafika mahali ambapo watu wapo huru kuvaa suruali bila ya kujali jinsia na atauhukumu wokovu wao based on mavazi bila  ya kuzingatia maudhui na maana hasa ya maandiko anayotumia.
Tuache kutiana hatia kwa mitazamo yetu binafsi isiyo na uhusiano wowote na Neno la Mungu.
NI HIVYO TU YAANI.

Maoni

  1. Sikubaliani na WW
    Vazi la kiume linajulikana mwanamke hasivae suruali Wala sketi za kubana Kama nguo ni shida ni afadhari kuacha kwa ajili ya wanaokwazika 2kor6:3-4

    JibuFuta
  2. Nakusihi uache injili nyepesi nyepesi

    JibuFuta
  3. Nakubaliana nawe unajua ubinafsi tu kwa mtazamo wangu unaleta hayo,,,wavae mavazi yanayostahili heshima.wajisitiri...wasiwaige makahaba wenye viwango hivyo vya kingono.

    JibuFuta
  4. Shida ni kutotambua kuwa Kwa Sasa hatuko chini ya Sheria bali chini ya Neema.Leo hii tunaongozwa Kwa Roho Mtakatifu na sio Sheria za mwanadamu.
    Unapovaa nguo kama mtu uliyeokoka, Roho Mtakatifu ndani yako anasemaje? Ukikosa amani,vua bali ukipata amani,ruksa. TAMANI KUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU NA SIO SHERIA ZILIZOTENGULIWA NA YESU

    JibuFuta
  5. Mimi naona tuangalie hili Mungu hana utamaduni,hizi tamaduni tulizonazo leo ktk makabila yetu au nchi zetu ni sisi ndio tumeziweka,hebu tuangalie kile kilicho kweli

    JibuFuta
  6. MIMI NAULIZA wewe mwanamke unaweza kuvaa suruwahi ukaenda kwenye nyumban ya Ibada Yaan kanisan
    mbona Huwa hatuwaon mkivaa hizo suruwal mnazosema za heshima mbona Huwa mbazivaa mtaan tu.. wewe uliyefundisha KUWA suruwal mwanamkeameruhisiwa unapotosha watu acha kupotosha watu Kwan kwa nyakat hiz mavaz ya mwanamke na mwanaume si yanajulikana

    JibuFuta

Chapisha Maoni